Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dharura ya mabadiliko ya tabianchi haina chanjo na haiwezi kusubiri tuchukue hatua sasa:UN

Hewa chafuzi ikitoka katika mtambo wa makaa ya mawe Kosovo
World Bank/Lundrim Aliu
Hewa chafuzi ikitoka katika mtambo wa makaa ya mawe Kosovo

Dharura ya mabadiliko ya tabianchi haina chanjo na haiwezi kusubiri tuchukue hatua sasa:UN

Tabianchi na mazingira

Wakuu wa nchi na serikali mbalimbali 77 wameungana na viongozi wa makampuni ya biashara na kutana leo Jumamosi kwa njia ya mtandao kuzungumzia malengo na matamanio ya mabadiliko ya tabianchi na ahadi mpya za kuyatimiza.

Mkutano huo“Matamanio ya mabadiliko ya tabianchi”viongozi wa masuala ya mabadiliko ya tabianchi wanauchukulia kwamba ni wenye malengo na matamanio makubwa zaidi duniani miongoni mwa serikali, makampuni na asasi za kiraia.

Lengo la mkutano huo ambao unaadhimisha miaka mitano baada ya makubaliano ya mkutano wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi ni kusaidia kutimiza malengo yaliyowekwa 12 Desemba 2015.

Mkutano huo ulioanza kwa kuonyeshwa video ya hali halisi ya mabadiliko ya tabianchi duniani kuanzia kuyeyuka kwa barabu, moto wa nyikani, majanga ya asili na kilio cha vijana cha kutaka hatua zichukuliwe umeandaliwa na Umoja wa Mataifa, serikali ya Uingereza na Ufanransa.

Washiriki

Mtazamo wa Ziwa Tanganyika upande wa Tanzania ambalo ukubwa wake umepungua kwa sababu mbali mbali ikiwemo shughuli za binadamu na mabadiliko ya tabianchi.
UN News/Assumpta Massoi
Mtazamo wa Ziwa Tanganyika upande wa Tanzania ambalo ukubwa wake umepungua kwa sababu mbali mbali ikiwemo shughuli za binadamu na mabadiliko ya tabianchi.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ni miongoni mwa washiriki wa mkutano huo akizungumza katika ufunguzi amesema”Miaka mitano baada ya mkutano wa Paris dunia bado haiku katika njia sahihi ya kutimiza malengo. Ahadi ya Pasris ni kudhibiti kiwango cha joto kusalia nyuzi joto 1.5C lakini ahadi iliyowekwa Paris haitoshi kufikia lengo n ahata ahadi hizo hazijatimizwa, viwango vya hewa ukaa hivi sasa viko katika viwango vya juu katika historia kwani tuko katika nyuzijoto 1.2C juu ya ilivyokuwa kabla mapinduzi ya viwanda.”

Kwa mantiki hiyo Katibu Mkuu amesisitiza“endapo hatutabadili mwelekeo tutakuwa tunaendelea kwenye kiwango cha joto ambacho ni zahma kubwa kikiongezeka kwa zaidi ya nyuzijoto 3C katika karne hii.Hivyo hakuna mashaka wala kupinga kwamba dunia hivi sasa inakabiliwa na dharura ya mabadiliko ya tabianchi.”

Hatua za kuchukua

Ukame barani Afrika utaathiri uzalishaji wa nafaka, imesema ripoti ya WMO iliyozinduliwa leo
WMO/Cornel Vermaak
Ukame barani Afrika utaathiri uzalishaji wa nafaka, imesema ripoti ya WMO iliyozinduliwa leo

Guterres ameongeza kuwa hadi sasa nchi 38 zimeshatangaza dharura ya mabadiliko ya tabianchi , wametambua uharaka na hatari iliyopo na ndio maaleo hii natoa wito kwa viongozi wote duniani kutangaza hali ya dharura ya mabnadiliko ya tabianchi katika nchi zao hadi pale utokomezaji wa hewa ukaa utakapotimia.

Katibu Mkuu amesema hatuko tayari kukusambaratishwa , juhudi za kujikwamua na janga la corona au COVID-19 zinatoa fursa ya kuziweka chumi na jamii zetu katika njia bora ya kuelekea kutimiza malengo ya ajenda ya 2030.

Hata hivyo ameonya kwamba“Hayo hayatokei na hadi sasa nchi wanachama wa G-20 wanatumia asilimia 50 zaidi ya fedha za kujikwamua katika sekta zinazohusiana na uzalishaji na matumizi ya mafuta kisukuku badala ya nishati zinazopunguza hewa ukaa. Hili ni suala lisilokubalika kwani matrilioni ya dola zinazohitajika kujikwamua na COVID-19 tunazikopa katika vizazi vijavyo na huu ni mtihani wa kimaadili.”

Ameongeza kuwa “Ili kufanya malengo kuwa hali halisi tunahitaji kuchukua hatua sasa kupunguza kiwango cha herwa chafuzi kwa asilimia 45 ifikapo mwaka 2045 na hay ani lazima yadhihirike katika malengo ya kila nchi NDC ambayo waliotia Saini mkataba wa Paris wanapaswa kuyawasilisha kabla ya COP26 hapo mwakani.

Msichana akipika katika moja ya vijiji nchini Ethiopia ambalo ardhi imeathirika vibaya na ukame unaoendelea
© UNICEF/Tanya Bindra
Msichana akipika katika moja ya vijiji nchini Ethiopia ambalo ardhi imeathirika vibaya na ukame unaoendelea

Washiriki

Miongoni mwa washiriki wengine katika mkutano huo ni wa wakuu wan chi na serikali 77 ni pamona na waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.

Pia wawakilishi kutoka asasi za kiraia wakiwemo wawakilishi kutoka jaa za watu wa asili na wawakilishi wa vijana ambao wamezungumzia jinsi gani mabadiliko ya tabianchi yanawaathiri.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa mkutano huo unaofanyika kwa njia ya mtandao“Ni hatua muhimu kulelekea mkutano wa 26 wa mabadiliko ya tabianchi COP26 utakaofanyika Novemba 2021 mjini Glasgow nchini Uingereza.

Wakati wa mwaka wa ukame, barafu zinazoyeyuka zinaweza kufikia asilimia 91 ya maji katika majiji kama Huaraz
UN News/Daniela Gross
Wakati wa mwaka wa ukame, barafu zinazoyeyuka zinaweza kufikia asilimia 91 ya maji katika majiji kama Huaraz

Umuhimu

Mkutano huu wa kimataifa unafanyika wakati dunia inapambana na janga la corona au COVID-19, lakini kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa “dunia inajua kwamba kwamba mabadiliko ya tabianchi hayana chanjo na hayawezi kusubiri hivyo mapencekezo ni kuchukua hatua sasa kwa Pamoja kwa ajili ya dunia ili kuweza kujikwamua vyema.Katika mkutano huu nchi zitaweka malengo na ahadi mpya chini ya nguzo tatu za mkataba wa Paris ambazo ni kudhibiti, kukabiliana na kufadhili vita dhidi ya janga hilo.”

Katibu Mkuu amesema mwaka ujao unatoa fursa nyingi za kukabiliana na dharura hii ya kimataifa kupitia mikutano mikubwa kwenye umoja wa Mataifa na mikakati mingine katika upande wa bayoanuai, bahari, usafiri, nishati, miji na nchi na mifumo ya chakula.