Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Biden airejesha Marekani WHO na mkataba wa Paris; UN yapongeza

Rais Joe Biden
UN Photo/Evan Schneider
Rais Joe Biden

Biden airejesha Marekani WHO na mkataba wa Paris; UN yapongeza

Tabianchi na mazingira

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, muda mfupi uliopita mjini New York Marekani, amekaribisha hatua ya Rais mpya wa Marekani Joe Biden kuirejesha Marekani katika Mkataba wa Paris mabadiliko ya tabianchi.

Hatua hiyo ya Biden inaifanya Marekani kuungana tena na muungano unaozidi kukua wa serikali, miji, mataifa, biashara na watu kote duniani ambao wanachukua hatua kabambe kukabiliana na tatizo la mabadiliko ya tabianchi.  

Kufuatia Mkutano wa matamanio ya Hali ya Hewa wa mwaka jana, nchi zinazozalisha nusu ya uchafuzi wa kaboni ulimwenguni zilikuwa zimejitolea kwa upande wowote wa kaboni. Kujitolea kwa leo na Rais Biden kunaleta takwimu hiyo kwa theluthi mbili. Lakini kuna njia ndefu sana ya kwenda. Mgogoro wa hali ya hewa unaendelea kuwa mbaya na wakati unazidi kupunguza kiwango cha joto hadi digrii 1.5 za Celsius na kujenga jamii zinazostahimili hali ya hewa ambayo husaidia kulinda walio hatarini zaidi. 

Kufuatia mkutano wa matamanio ya tabianchi uliofanyika mwaka jana 2020, nchi zinazozalisha nusu ya hewa chafuzi ya ukaa ulimwenguni, zilijitolea kuidhibiti hewa ukaa.  

Bwana Guterres amesema, “kujitolea kwa leo kwa Rais Biden kunaleta takwimu hiyo kuwa theluthi. Lakini kuna njia ndefu sana ya kwenda. Janga la tabianchi linaendelea kuwa baya na muda unayoyoma, kuweza kudhibiti ongezeko la joto kufikia nyuzi joto 1.5 na kujenga jamii zenye mnepo wa tabianchi ili kuwlinda waliko hatarini zaidi.”  

Aidha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema anaahidi kufanya kazi kwa karibu na Rais Biden na viongozi wengine kuishinda dharura ya tabianchi na kupona vizuri dhidi ya COVID-19.   

Mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi unatarajiwa kuanza kwa kutekelezwa nchini Marekani tarehe 19 mwezi ujao wa Februari kwa mujibu wa Ibara namba 21 kipengele(3)

Marekani ilijiunga na mkataba huo tarehe 22 mwezi Aprili mwaka 2016 na kuelezea nia yake ya kuanza kuutekeleza tarehe 3 Septemba mwaka 2016 kabla ya kujitoa tarehe 4 Novemba mwaka 2020.

Kuhusu WHO 

Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu Guterres kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake mjini New York Marekani, amekaribisha hatua ya Marekani kurejesha ushirikiano na shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO.  

Katibu Mkuu Guterres amesema kuisaidia WHO ni muhimu kwa juhudi za ulimwengu kwa ajili ya mapambano yaliyopangwa vema dhidi ya COVID-19.  

“Hivi sasa ni wakati wau moja na jumuiya ya kimataifa kufanya kazi pamoja kwa mshikamano ili kuzuia virusi na madhara yake makubwa.” Amesema Guterres. 

Aidha Guterres amesema chanjo ikiwa nyenzo muhimu katika vita dhidi ya COVID-19, Marekani ikijiunga na kusaidia kituo cha COVAX itaongeza kasi kwa juhudi za kuhakikisha upatikanaji wa chanjo sawa kwa nchi zote.