Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Tanzania na harakati za kuimarisha huduma ya haki kwa wananchi

Upatikanaji wa haki na amani kwa wote ni lengo namba 16 katika malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa, SDGs.

Umoja wa Mataifa umetambua kwamba vyombo vya sheria viko katika hatari kubwa ya kukumbwa na ufisadi, na Tanzania imeweka mikakati ya kukabiliana na suala hili ana kwa ana. Ni kwa mantiki hiyo ambapo Tanzania imeweka kipaumbele kukarabati upya sekta ya haki kwa kusambaza huduma kote nchini, ili kuwafikia wale ambao kwa muda hawajapata huduma hiyo.

Basi ungana na Grace Kaneiya kwa undani zaidi, katika makala hii.

Hafla ya kuenzi Kichina yapambwa kwa burudani ya muziki

Lugha ni kiungo muhimu katika utamaduni kwani inakuwa ni moja ya utambulisho wa watu wenye asili moja. Umoja wa Mataifa kwa kutambua umuhimu wa lugha umeanzisha programu ya kutoa mafunzo ya lugha mbali mbali kutoka mabara tofauti duniani.

Moja ya lugha ambazo zinafundishwa katika Umoja wa Mataifa ni Kichina, programu ambayo hivi karibuni imeadhimisha miaka 14 tangu kuasisiwa.

Matumizi sahihi ya barabaraba kwa vyombo sahihi yahitajika Bujumbura

Wiki ya usalama baranarani ikiendelea shirika la afya ulimwenguni WHO, linapendekeza pamoja na mambo mengine, uboreshaji wa miundombinu ya barabara ili kupunguza ajali.

Nchini Burundi hatua zaidi zinahitajika ili kudhibiti matumizi sahihi ya barabara baina ya baiskeli na magari pamoja na watumiaji wengine wa barabara wakiwamo watembea kwa miguu ili kudhibiti ajali za barabarani.

Mwandishi wetu Ramadhani Kibuga, amevinjari mjini Bujumbura na kuandaa makala ifuatayo. Ungana naye.

WFP na wadau wahaha kusaidia CAR inapokumbwa na mzozo wa kibinadamu

Tangu machafuko yalipozuka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), taifa hilo limejikuta katika mzozo wa kibinadamu unaoendelea. Lakini mzozo wa nchi hiyo ni moja ya mizozo ya kibinadamu iliyosahaulika ulimwenguni, na kwa mujibu wa Shirika la Mpango wa Chakula Ulimwenguni (WFP), ufadhili kwa ajili ya usaidizi wa kibinadamu unazidi kudidimia. Kwa mfano, WFP inasema mpango wake wa shughuli za kibinadamu kwa mwaka 2017, umefadhiliwa kwa asilimia saba tu kufikia sasa.

Nuru yaangazia familia za wakimbizi Ureno

Familia kadhaa za wakimbizi kutoka Iraq na Palestina zimanufaika na ukarimu kutoka kwa moja ya miji nchini Ureno, ambapo mamlaka mjini humo imeonyesha ukarimu kwa kuwahifadhi na kukidhi haja zao.

Hatua hii inaunga mkono juhudi za Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR linalofanya kazi ya kulinda na kusaidia wale wanaokimbia vita na mateso tangu mwaka 1950.

Hadi sasa shirika hilo limefanikiwa kurejesha matumaini kwa mamilioni ya wakimbizi ulimwenguni kote.

Ungana na Amina Hassan katika makala ifuatayo kufahamu.

Uhuru wa vyombo vya habari wamulikwa hususan Afrika Mashariki

Ulimwengu umeadhimisha mapema wiki hii siku ya uhuru wa vyombo vya habari,  sherehe za siku hiyo kimataifa zikifanyika huko Jakarta, Indonesia, zikiratibiwa na  shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO.

Katika ujumbe wake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António  Guterres alisema bado wanahabari wanakumbwa na vitisho, mashambulizi ya kingono, kujeruhiwa, kutiwa korokoroni na hata kuuawa.

Shilingi moja ya leo ni mbili ya kesho (Sehemu ya pili)-Kijana mfuga sungura

Karibu katika sehemu ya pili ya mahojiano baina ya Peter Kagereki, kijana aliyevunja mipaka ya utamaduni wa vijana wengi wasomi barani Afrika kusubiri ajira za ofisini.

Yeye ni miongoni mwa washindi watatu wa shindano la benki ya dunia kuhusu matumizi ya blogu kwa maendeleo, #Blog4Dev. Kagereki anasema sungura anaofua humpatia kipato asilani, kwani huuza mbolea itokanayo na wanyama hao.

Kwa undani zaidi sikiliza sehemu ya pili ya mahojiano yake na Grace Kaneiya.

Shilingi moja ya leo ni shilingi mbili ya kesho: Kijana mfuga Sungura

Si kawaida sana kwa msomi barani Afrika kufanya kazi ya ufugaji tena kufuga sungura. Hii ni tofauti kwa kijana Peter Kagereki kutoka Kenya ambaye ni miongoni mwa washindi watatu watatu wa shindano la benki ya dunia kuhusu matumizi ya blogu kwa maendeleo, #Blog4Dev. Kagereki pamoja na mambo mengine anasema kauli ya mwalimu wake kuhusu uwekezaji akitumia mfano wa shilingi, imemwezesha kuwa mfugaji aliyejipatai kipato na kwa kutumia msaada wa teknolojia anasonga mbele.

Kwa undani zaidi sikiliza sehemu ya kwanza ya mahojiano yake na Grace Kaneiya.

Hatimiliki huwezesha ubunifu kunufaisha jamii-WIPO

Aprili 26 ni siku ya hatimiliki duniani ambako katika kuadhimisha siku hii Mkurugenzi mkuu wa  shirika la kimataifa la hatimiliki, WIPO, Francis Gurry amesema, hatimiliki ni sehemu muhimu ya sekta ya ubunifu na ina faida kwa wale wanaochukua fursa ya kuzindua bidhaa mpya na huduma katika uchumi.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Ubunifu- kuimarisha maisha” ambako Bwana Gurry amesema licha ya kwamba ubunifu unaimarisha maisha yetu, mara nyingi jamii haichukui muda kutafakari jinsi ubunifu ulivyobadilisha kiwango cha maisha.