Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhuru wa vyombo vya habari wamulikwa hususan Afrika Mashariki

Uhuru wa vyombo vya habari wamulikwa hususan Afrika Mashariki

Pakua

Ulimwengu umeadhimisha mapema wiki hii siku ya uhuru wa vyombo vya habari,  sherehe za siku hiyo kimataifa zikifanyika huko Jakarta, Indonesia, zikiratibiwa na  shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO.

Katika ujumbe wake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António  Guterres alisema bado wanahabari wanakumbwa na vitisho, mashambulizi ya kingono, kujeruhiwa, kutiwa korokoroni na hata kuuawa.

Kwa mantiki hiyo, Bwana Guterres alisema huu ni wakati wa kila mtu kusimama kidete kutetea wana tasnia hiyo kwa lengo la kuepusha utoaji habari zisizo sahihi.

Photo Credit
Waandishi wa habari.(Picha:UM/Isaac Billy)