Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hafla ya kuenzi Kichina yapambwa kwa burudani ya muziki

Hafla ya kuenzi Kichina yapambwa kwa burudani ya muziki

Pakua

Lugha ni kiungo muhimu katika utamaduni kwani inakuwa ni moja ya utambulisho wa watu wenye asili moja. Umoja wa Mataifa kwa kutambua umuhimu wa lugha umeanzisha programu ya kutoa mafunzo ya lugha mbali mbali kutoka mabara tofauti duniani.

Moja ya lugha ambazo zinafundishwa katika Umoja wa Mataifa ni Kichina, programu ambayo hivi karibuni imeadhimisha miaka 14 tangu kuasisiwa.

Hafla hiyo iliwakutanisha watu mbali mbali akiwemo mwanamuziki Ma Lin kutoka China, yeye ni mcheza ala yenye asili ya China! Basi ungana na Grace Kaneiya katika Makala ifuatayo kwa undani wa muziki anaocheza bi. Lin

Photo Credit
Mwanaumuziki wa Pipa, Ma Lin katika Umoja wa Mataifa.(Picha:UM/Video capture)