Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Nilitembea kutwa kucha na wanangu kutoka Sudan Kusini hadi Uganda kunusuru maisha-Sehemu ya 2

Kutana na Jade Kide katika sehemu ya pili ya mahojiano na John Kibego.  Yeye ni mama wa watoto wanne na amehaha kusaka hifadhi na kujikuta akitembea usiku na mchana kutoka Sudan Kusini kukimbia machafuko.

Amewasili Uganda katika kambi ya wakimbizi ya Kiryandongo, akiwa ametokea jimboni Equatoria Mashariki nchini Sudan Kusini. Anasilimulia kadhia zinazomakabili akikumbuka namna alivyompoteza mwanae na wazazi kufuatia mgogoro nchini mwake.

Nilitembea kutwa kucha na wanangu kutoka Sudan Kusini hadi Uganda kunusuru maisha-Sehemu ya 1

Kutana na Jade Kide, mama wa watoto wanne, ambaye amehaha kusaka hifadhi na kujikuta akitembea usiku na mchana kutoka SudanKusini kukimbia machafuko.

Amewasili Uganda katika kambi ya wakimbizi ya Kiryandongo, akiwa ametokea jimboni Equatoria Mashariki nchini Sudan Kusini. Anasilimulia kadhia zinazomakabili akikumbuka naman alivyompoteza mwanae na wazazi kufuatia mgogoro nchini mwake.

John Kibego anazungumza naye katika sehemu ya kwanza ya makala hii.

Nimetumikishwa kama kahaba, nashindwa kujinasua-Joy

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF inasema mamilioni ya watoto wanavuka mipaka ya kimataifa wakikimbia vurugu na migogoro, majanga au umaskini wakitumainia kupata maisha bora ugenini.

Shirika hilo linasema katika mwaka 2015 - 2016, Idadi ya watoto wakimbizi na wahamiaji waliotenganishwa na wasioambatana na wazazi wao ilifikia 300,000 kutoka nchi 80 ikilinganishwa na 66,000 katika mwaka 2010 – 2011.

Ulemavu sio ukosefu wa uwezo

Ulemavu sio ukosefu wa uwezo, ndivyo unavyoweza  kusema ukisikiliza kipaji cha muziki cha mwanadada Bogdana Petrova mwenye ulemavu wa kutoona kutoka nchini Bulgaria.

Nyota huyu aliyewashangaza wengi kwa uwezo wake bila kujali hali yake, ametoa burudani juma hili mjini New York. Joseph Msami amefuatilia tukio hilo na kukuandalia makala ifuatayo.

Natamani wasio walemavu wavae viatu vyetu: Mwakilishi walemavu Tanzania

Kila anayetunyima fursa tunatamani angevaa viatu vyetu, ahisi uchungu tunaopitia, ni kauli ya mmoja wa wawakilishi wa watu wenye ulemavu kutoka Tanzania Zanzibar Bi Abeida Rashid Abdallah, Mkurugenzi Idara ya Watu wenye ulemavu kwenye ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

Bi Abeida anyehudhuria mkutano wa 10 wa nchi wanachama wa mkataba wa watu wenye ulemavu CRPD, unaomalizika juma hili mjiniNew York, amemweleza Joseph Msami katika mahojiano maalum kwamba wanachokihitaji ni kuona mkataba huo ambao Tanzania imeridhia unatakelezwa.

Ushirika waleta nuru kwa wakimbizi Uganda

Nchini Uganda, kitendo cha nchi hiyo kuwezesha wakimbizi kutangamana na wenyeji katika shughuli za kujikwamua kiuchumi, kimeleta ahueni kubwa kwa wakimbizi, fursa ambayo ni nadra sana kuipata kwingineko wanakopatiwa hifadhi,. Uganda pamoja na kuwezesha wakimbizi kupata ardhi ya kulima na hata kujenga makazi, sasa inaruhusu wenyeji na wakimbizi kujiunga katika vikundi vya ushirika ambavvyo kwavyo vinaleta pamoja stadi mbali mbali na kuboresha maisha. Je nini kinafanyika? Ungana basi na John Kibego kwenye makala hii.

Kutoboka kwa kiatu si mwisho wa safari

Nchi ya Uganda inasifiwa kwa kupokea wakimbizi wengi na kuwajumuisha katika jamii kwa kuwapa kazi, ardhi na fursa za kujiendeleza. Mbali na changamoto nyingi anazokumbana nazo , mmoja wa wakimbizi hao anatumia fursa hiyo kujisaidia na kuwasaidia wengine. Sikiliza makala hii ya Amina Hassan yenye kusimulia zaidi.

Uhifadhi wa mazingira hususan Afrika

Mapema juma hili, dunia imeadhimisha siku ya mazingira, siku ambayo huadhimishwa Juni tano ya kila mwaka. Ujumbe wa mwaka huu ni utengamano na asili, ukilenga kuhakikisha ulinzi wa maliasili za mazingira ili kukuza uendelevu wa viumbe na sayari dunia.

Shirika la mpango wa mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP na wadau  wake,  wametumia maadhimisho hayo kufikisha ujumbe juu ya  kuithamini dunia kwa kulinda mazingira dhidi ya changamoto za uharibifu.

Dunia itupie macho visiwa vya Afrika kulinda bahari: Dk Tizeba

Macho yote yameelekezwa kwenye visiwa vya Magharibi, hili lapaswa kukoma! Ni kauli ya Waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi wa Tanzania Dk Charles Tizeba wakati akihutubia mkutano wa kimataifa kuhusu bahari unaoendelea mjini New York.

Katika mahojiano maalum na Joseph Msami wa idhaa hii, Dk Tizeba ameitaka jumuiya ya kimataifa kutozisahau nchi zinazoendelea zenye visiwa ambazo zaweza kunufaika kiuchumi na kijamii na uwepo wa bahari.

Afrika inahitaji mageuzi katika amani-Mongella

Baada ya kuundwa na kukutana mjini New York Marekani kwa siku tatu, mtandao wa viongozi wanawake wa Afrika, umeazimia pamoja na mambo mengine kuhakikisha bara hilo linajikomboa katika migogoro kisha kupiga hatua za kimaendeleo.

Miongoni mwa waliohuduhuria mkutano huo ni mwanasiasa nguli kutoka Tanzania, aliye pia mwanaharakati wa wanawake, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Advocacy for Women in Africa Bi Gertrude Mongella,aliyemweleza Joseph Msami muda mfupi baada ya mkutano kuwa ipo fursa ya ukombozi wa wanawake katika maeneo yenye migogoro.