Shilingi moja ya leo ni shilingi mbili ya kesho: Kijana mfuga Sungura
Pakua
Si kawaida sana kwa msomi barani Afrika kufanya kazi ya ufugaji tena kufuga sungura. Hii ni tofauti kwa kijana Peter Kagereki kutoka Kenya ambaye ni miongoni mwa washindi watatu watatu wa shindano la benki ya dunia kuhusu matumizi ya blogu kwa maendeleo, #Blog4Dev. Kagereki pamoja na mambo mengine anasema kauli ya mwalimu wake kuhusu uwekezaji akitumia mfano wa shilingi, imemwezesha kuwa mfugaji aliyejipatai kipato na kwa kutumia msaada wa teknolojia anasonga mbele.
Kwa undani zaidi sikiliza sehemu ya kwanza ya mahojiano yake na Grace Kaneiya.