Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Uhifadhi wa kompyuta au simu wachangia uhifadhi wa mazingira Burundi

Kawaida likija swala la  kuhifadhi mazingira , katika nchi zinazoendelea  watu hufikiria haraka swala la  mabadiliko ya tabia nchi na uchafuzi wa hewa ikiwemo uhifadhi wa miti , mito na kadhalika. lakini je  unajua  kuwa uhifadhi wa komputa au simu ni moja  ya mikakati ya kuhifadhi vyema mazingira? Nchini Burundi , sehemu nyingi  na ofisini hamna  utaratibu wa kuhifadhi komputa na simu za mikononi au rununu, na hivyo hali hiyo kuonekena kama ni kitisho kikubwa cha mazingira na afya.

Athari za matumizi ya tumbaku kwa jamii na watu binafsi

Mei 31 kila mwaka ni siku ya kupiga marufuku matumizi ya tumbaku duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni  “Tumbaku- tishio dhidi ya maendeleo”.

Shirika la afya ulimwenguni WHO limesema kwamba zaidi ya watu milioni 7 hufariki dunia kila mwaka huku ikigharimu familia na serikali takriban dola trilioni 1.4 kwa ajili ya matibabu na nguvu kazi.

Hatua za upasuaji kwa wagonjwa Fistula -sehemu ya Pili

Katika sehemu hii ya pili na ya mwisho ya mahojiano na mtaalamu wa afya kutoka mkoani Kagera nchini Tanzania  Dk Martin Lwabilimbo, tunaelezwa kile ambacho kinafanyika baada ya upasuaji wa kurekebisha Fistula, ugonjwa ambao unaondoa utu wa mwanamke. Mathalani Dokta Lwabilimbo amemweleza Nicolaus Ngaiza wa Radio washirika Kasibante FM mkoani humo kuwa, mgonjwa akishafanyika upasuaji anapatiwa pia ushauri nasaha ili aweze kurejea katika hali ya kawaida na kujitambua kwa kuwa awali kabla ya upasuaji huwa wanapoteza hata hali ya kujiamini na kutangamana na watu. Dkt.

Hatua za upasuaji kwa wagonjwa Fistula -sehemu ya kwanza

Ugonjwa wa Fistula ambao huwakumba akina mama pindi wachelewapo kupata huduma wakati wa kujifungua ni changamoto hususan nchi zinazoendelea.

Hatua ya upasuaji dhidi ya wagonjwa wa Fistula hufanywa pale inapobidi kuokoa maisha ya mgonjwa. Katika sehemu ya kwanza ya makala ifuatayo Nicolaus Ngaiza wa redio washirika Kasibante Fm ya Kagera Tanzania anazungumza na Dk Martin Lwabilimbo kutoka idara ya upasuaji hospitali ya rufaa ya mkoa huo. Awali Dk Lwabilimbo anafafanua maana ya upasuaji huo.

Mwongozo wa kilimo salama Tanzania ni nuru kwa wakulima, wafugaji na wavuvi

Nchini Tanzania kuanzia tarehe 31 mwezi Mei mwaka 2017, Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi inaanza kuelimisha watendaji wake katika halmashauri jinsi ya utekelezaji wa mwongozo mpya wa kilimo salama uliozinduliwa mwishoni mwa wiki. Mwongozo huo ukiambatana na wasifu wa kilimo salama kinachohimili mabadiliko ya tabianchi unalenga kupunguza, kuhimili na kukabili athari za mabadiliko ya tabianchi katika sekta za kilimo, ufugaji na uvuvi.

Makala ya wiki: Ugonjwa wa Fistula

Fistula!  Ugonjwa unaoathiri wanawake takriban milioni mbili katika nchi zinazoendelea, wanawake ambao huteseka wakijificha kwa aibu na kunyanyapaliwa. Katika maadhimisho ya Siku ya Kukomesha Fistula Duniani, yenye maudhui ya “Matumaini, Uponyaji, na Heshima kwa Wote”, Shirika la Idadi ya Watu, UNFPA limetoa wito wa kutambua haki za msingi za binadamu kwa waathirika ambao idadi yao kubwa ni masikini, kwani ugonjwa huu ni rahisi kutibika, na umetokomezwa katika mataifa yaliyoendelea.

Fahamu umuhimu wa huduma ya Kangaroo kwa mtoto njiti

Huduma ya Kangaroo ambayo hujulikana pia kama huduma ya ngozi-kwa-ngozi ni huduma iliyoanzishwa miaka ya 70 kuokoa maisha ya watoto njiti katika sehemu ambazo vifaa vya unyevunyevu kwa mtoto njiti au incubator havipatikani au kutumika. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF linasema watoto hawa njiti huzaliwa na miili dhaifu na hivyo kuwaweka hatarini zaidi kupoteza maisha yao iwapo hawatapa huduma hii kwa haraka na kwa usanifu.

Wimbo maalum wa kuanikiza kazi za UM

Ni kawaida wanamuziki kurekodi nyimbo studio na kutumia maeneo kama vile kumbi mbalimbali za starehe kutumbuiza. Lakini hilo limekuwa tofauti kwa kundi la moja la muziki ambalo lilibisha hodi makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani, na kurekodi wimbo maalum.

Ni wimbo wa historia na kazi za Umoja wa Mataifa . Amina Hassan anakuletea makala maalum kuhusu wimbo huo.Ungana naye.

Familia na makuzi yake hususan nchini Uganda

Familia!  Msingi bora wa jamii na taifa kwa ujumla.Kuna usemi usemao, Taifa bora hujengwa na familia bora. Kwa kutambua hilo, Umoja wa Mataifa unaenzi familia kwa kuadhimisha siku ya duniani kila tarehe 15 ya mwezi Mei. Mwaka huu ujumbe ni Familia, elimu na ustawi.

Maadhimisho yanalenga katika jukumu la taasisi hiyo na sera za kukuza elimu na kwa ujumla ustawi wa familia. Kwa ujumla siku hii inajikita katika kuelimisha familia katika kukuza elimu utotoni pamoja na fursa za muda mrefui kwa mtoto na kijana.

Msichana wa Kisomali aonyesha jinsi azma na uthabiti inavyoweza kubadili maisha

Iqra Ali Omar, msichana mwenye umri wa miaka 19, alianza kuishi na jamaa zake, wazazi wake walipoachana akiwa mtoto mdogo sana.

Isingalikuwa kwa ajili ya moyo wake thabiti, hatma yake ingalikuwa kama ya wasichana wengine wengi wa Kisomali, ambao kawaida hulazimishwa na familia zao maskini kuingia ndoa za utotoni.

Baada ya serikali ya kitaifa ya Somalia kusambaratika mnamo mwaka 1991, jukumu la Wizara ya Elimu lilichukuliwa na taasisi za kibinafsi, ambazo zilisajili na kutoa huduma za elimu ya malipo kwa watoto wenye umri wa kwenda shule.