Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COP26

COP26: 31 Oktoba-12 Novemba 2021 | Glasgow, Uingereza

Kwa takribani miongo mitatu, Umoja wa Mataifa (UN) umekuwa ukileta pamoja kila nchi duniani kwenye mikutano ya ngazi ya juu kuhusu tabianchi, mikutano ikipatiwa jina COP yaani conference of Parties kwa kiswahli wanachama wa mkutano. Tangu wakati huo, mabadiliko ya tabianchi yamebadilika kutoka suala la  pembezoni hadi kipaumbele cha kimataifa.
 
Mwaka huu utakuwa mkutano wa 26 wa nchi wanachama wa mikutano hiyo, ikipatiwa jina COP26. Uingereza ndio Rais wa mkutano hou wa COP26 na unafanyika Glasgow, Scotland.
Kuelekea COP26, Uingereza inafanya kazi na kila taifa kufikia makubaliano ya jinsi ya kukabili mabadiliko ya tabianchi. Viongozi wa dunia wanawasili Scotland, sambamba na makumi ya maelfu ya washauri, wawakilishi wa serikali, sekta ya biashara, wananchi kwa ajili ya mkutano huo wa siku 12.
Si tu kwamba ni jukumu kubwa, bali pia ni tofaauti na mikutano mingine iliyotangulia ya nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi. Wataalamu wengi wanaamini kuwa COP26 ni dharura ya kipekee.
Ili kupokea taarifa za kila wakati moja moja kwenye akaunti yako ya barua pepe, tafadhali hakikisha  unajisajili hapa kwenye mada kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi

Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Tabianchi.
UN /Cia Pak

Madhara ya tabianchi yanachanja mbuga, hatua kwa tabianchi zinadorora- UN

Wawakilishi wa serikali wakianza kukamilisha ajenda kwa ajili ya mkutano wa 27 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Kimataifa wa mabadiliko ya tabianchi, COP27 utakaofanyika mwezi ujao huko Misri, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewaambia waandishi wa habari jijini New York, Marekani kuwa kazi iliyo mbele ni kubwa na nzito wakati huu ambapo madhara ya tabianchi yanashuhudia kote duniani.

Kutokana na mabadiliko ya tabianchi, jamii ya wafugaji, Maasai wa Loliondo kaskazini mwa Tanzania wamelazimika kuhamia katika kilimo.
Mathias Tooko

Mabadiliko ya tabiachi yaanza kubadilisha maisha ya jamii ya Maasai, Loliondo, Tanzania

Watu jamii ya Maasai huko Loliondo, wilaya ya Ngorongo, Tanzania ambao kwa miaka yote ya uwepo wao shuguli yao ya kujipatia kipato na chakula ni kupitia mifugo hususani ng’ombe, na chakula chao ni nyama na maziwa, sasa wameanza kulazimika kuanza kuhamia katika shughuli za kilimo baada ya shughuli yao hiyo ya  asili ufugaji kuathiriwa na mabadiliko ya tabianchi. 

31 DESEMBA 2021

Katika jarida la matukio ya mwaka la Umoja wa Mataifa hii leo Assumpta Massoi anakuletea

-Wanajeshi watatu wa kulinda amani kutoka Tanzania wanaohudumu kwenye mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati MINUSCA, wamejeruhiwa na mmoja vibaya sana baada ya msafara wao kukanyaga vilipuzi. Wote wanatibiwa hospitalini mjini Bangui

-Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema mwaka huu umekuwa wa machungu na ukiukwaji mkubwa wa haki za watoto katika mizozo ya muda mrefu na ile mipya. 

Sauti
12'7"

12 Novemba 2021

Karibu kusikiliza jarida ambapo leo Mada yetu kwakina inatokea huko Glasgow Scotland ambapo mkutano wa 26 wa nchi wanachama wa mkataba wa  mabadiliko ya tabianchi COP26 ukiwa unafunga pazia mwanaharakati wa Mazingira Dkt. Sixbert Mwanga kutoka nchini Tanzania anasema Afrika pamoja na kuwa na kauli moja lakini haijafanikiwa kwenye mkutano huo.

Pia utasikia habari kwa ufupi na kupata fursa ya kujifunza kiswahili .

Sauti
9'56"
Basi la National Express lisilotoa hewa chafuzi likiwa nje ya Mkutano wa mabadiliko ya tabianchi COP26 huko Glasgow, Scotland.
UN News/Laura Quinones

Wakati umefika kugeukia usafiri unaolinda mazingira: COP26

Kuwa na dunia ambayo vyombo vya usafiri kama magari, mabasi na malori ambayo yanatumia umeme n ani ya gharama nafuu, kuwa dunia ambayo vyombo wa usafiri wa bahari vinatumia nishati safi pekee na ndege ziweze kusafiri kwa kutumia hewa safi ya Hydrogen inaweza kuonekana kama ndoto ama sinema lakini kwenye mkutano wa COP26 unaoendelea huko Glasgow serikali nyingi na makampuni ya biashara wamesema wameanza kutimiza ndoto hizi na kuzifanya kuwa hali halisi.