Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

31 DESEMBA 2021

31 DESEMBA 2021

Pakua

Katika jarida la matukio ya mwaka la Umoja wa Mataifa hii leo Assumpta Massoi anakuletea

-Wanajeshi watatu wa kulinda amani kutoka Tanzania wanaohudumu kwenye mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati MINUSCA, wamejeruhiwa na mmoja vibaya sana baada ya msafara wao kukanyaga vilipuzi. Wote wanatibiwa hospitalini mjini Bangui

-Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema mwaka huu umekuwa wa machungu na ukiukwaji mkubwa wa haki za watoto katika mizozo ya muda mrefu na ile mipya. 

-Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limesitisha opetresheni zake jimboni Darfur Kaskaini nchini Sudan baada ya mabohari yake matatu kuporwa mjini El Fasher hali ambayo itaathiri watu milioni 2 wanaohitaji msaada nchini humo mwaka 2022

-Mada kwa kina leo inamulika matukio makubwa yaliyojiri mwaka 2021

-Na katika kujifunza Kiswahili leo tuko Kenya kwa mtalam wetu Josephat Gitonga akifafanua methali ""IMARA YA JEMBE KAINGOJE SHAMBANI"

Audio Credit
UN News/Assumpta Massoi
Sauti
12'7"