Kwa takribani miongo mitatu, Umoja wa Mataifa (UN) umekuwa ukileta pamoja kila nchi duniani kwenye mikutano ya ngazi ya juu kuhusu tabianchi, mikutano ikipatiwa jina COP yaani conference of Parties kwa kiswahli wanachama wa mkutano. Tangu wakati huo, mabadiliko ya tabianchi yamebadilika kutoka suala la pembezoni hadi kipaumbele cha kimataifa.
Mwaka huu utakuwa mkutano wa 26 wa nchi wanachama wa mikutano hiyo, ikipatiwa jina COP26. Uingereza ndio Rais wa mkutano hou wa COP26 na unafanyika Glasgow, Scotland.
Kuelekea COP26, Uingereza inafanya kazi na kila taifa kufikia makubaliano ya jinsi ya kukabili mabadiliko ya tabianchi. Viongozi wa dunia wanawasili Scotland, sambamba na makumi ya maelfu ya washauri, wawakilishi wa serikali, sekta ya biashara, wananchi kwa ajili ya mkutano huo wa siku 12.
Si tu kwamba ni jukumu kubwa, bali pia ni tofaauti na mikutano mingine iliyotangulia ya nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi. Wataalamu wengi wanaamini kuwa COP26 ni dharura ya kipekee.
Ili kupokea taarifa za kila wakati moja moja kwenye akaunti yako ya barua pepe, tafadhali hakikisha unajisajili hapa kwenye mada kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi
COP26
05 Novemba 2021
Karibu kusikiliza jarida ambapo leo ni siku ya kimataifa ya uelimishaji kuhusu Tsunami, na kama ilivyo ada leo ni mada kwa kina ambapo tunaangazia vijana na mchango wao katika mabadiliko ya tabianchi wakati mkutano wa Umoja wa Mataifa COP26 ukiendelea huko Glasgow Scotland.
Flora Nducha amezungumza na mmoja wa vijana wanaharakati wa mazingira kutoka nchini Kenya na mshindi wa tuzo ya shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP ya champion of the Earth 2020 kutokana na kampuni yake ya Change Makers kubadili taka za platiki kuwa tofali.
Vijana tunaweza ni wakati wa kutushirikisha kwa vitendo katika vita dhidi ya mabadiliko ya tabianchi:Nzambi
Wakati mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP26 ukiendelea mjini Glasgow Scotland, vijana wanatoa wito kwa viongozi kutekeleza kwa vitendo ushirikishwaji wa vijana katika vita dhidi ya janga hilo.
Siku ya nishati COP26 yasikia vilio vya kutaka makaa ya mawe yasalie historia
Katika siku ya nne ya mkutano wa 26 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP26 huko Glasgow, Scotland, sauti zimepazwa na wanaharakati wakitaka kukomeshwa kwa matumizi ya makaa ya mawe nishati ya gesi na mafuta, sauti ambazo zimepaswa siku ambayo mkutano huo ulikuwa unamulika nishati.
Mauritania wapambana na mabadiliko ya tabianchi
siku chache kabla ya kuanza kwa mkutano huo wa 26 wa nchi wanachama wa mabadiliko ya tabianchi, ambao hivi sasa unaendelea Glascow, Scotland, Mshauri Maalumu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudunia wakimbizi, UNHCR kuhusu Hatua dhidi ya Mabadiliko ya Tabianchi, Andrew Harper ametembelea Mauritania kujionea jinsi wakimbizi wanavyopambana na janga la tabianchi.
(Taarifa ya John Kibego)
“Hatujawahi kuona mwaka kama 2021. Huu ni mwaka wenye mioto mingi ya nyika.” Anasema Ahmedou El-Bokhary, Rais wa Kikosi cha zima moto kinachoundwa na wakimbizi.
04 Novemba 2021
Karibu kusikiliza jarida, leo ni siku ya kimataifa ya kupinga uonevu shuleni na mitandaoni ambapo UNESCO imetaka watoto kulindwa zaidi, WFP imetoa msaada kwa wananchi wa Madagascar wanaoishi katika ukame na hivyo kulazimika kula mmea wa Dungusi kakati.
Pia utasikia kauli ya Rais wa COP26 huko Glasgow kuhusu nchi tajiri kutoa fedha za kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Kama sisi tumeweza, wengine washindwe kwa nini? – Wakimbizi Mauritania
Hivi karibuni, siku chache kabla ya kuanza kwa mkutano wa 26 wa nchi wanachama wa mabadiliko ya tabianchi, #COP26 ambao hivi sasa unaendelea Glascow, Uskochi, Mshauri Maalumu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudunia wakimbizi, UNHCR kuhusu Hatua dhidi ya Mabadiliko ya Tabianchi, Andrew Harper ametembelea Mauritania kujionea jinsi wakimbizi wanavyopambana na janga la tabianchi.
Mtanzania Imani Nsamila mpigapicha za mazingira, ashinda tuzo ya EU GCCA+
Kijana Mtanzania mpigapicha za mazingira Imani Nsamila ametangazwa kuwa mshindi wa Tuzo za Vijana za EU GCCA+ zinazolenga kuwasaidia wanahabari wachanga, waandishi na wapiga picha kusimulia taarifa au simulizi zenye nguvu za tabianchi kote ulimwenguni.
COP26: Hakuna tena maneno matupu, sekta binafsi zajitoa kimasomaso- Carney
Katika siku inayomulika sekta ya fedha na udhibiti wa mabadiliko ya tabianchi kwenye mkutano wa 26 wa nchi wanachama wa mabadiliko ya tabianchi, COP26 huko Glasgow, Scotland, takribani kampuni binafsi 500 zimekubaliana kutenga dola trilioni 130 kutekeleza mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi ikiwemo hakikisha kiwango cha joto duniani hakizidi nyuzijoto 1.5 katika kipimdo cha Selsiyasi.
3 Novemba 2021
Karibu katika jarida ambapo utasikia kuhusu ushindi wa kijana mtanzania katika tuzo zilizotolewa leo sanjari na mkutano wa 26 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP26.
Habari kwa ufupi leo zimeangazia ripoti ya uchuguzi wa masuala ya haki za binadamu huko Tigray nchini Ethiopia na baa la njaa nchiniMadagascar
Zaidi ya nchi 100 zimeahidi kusitisha na kubadilisha ukataji miti ifikapo 2030
Azimio la kihistoria la kuokoa na kurejesha misitu ya dunia katika ubora wake limetangazwa leo rasmi katika siku ya pili ya mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi unaoshirikisha viongozi wa dunia au COP26.