Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ili kutimiza lengo la mabadiliko ya tabianchi lazima tutimize lengo la misitu:FAO/UNECE

Ukataji miti ni ubadilishaji wa misitu kuwa matumizi mengine ya ardhi, kama vile kilimo na miundombinu.
©FAO/Karen Minasyan
Ukataji miti ni ubadilishaji wa misitu kuwa matumizi mengine ya ardhi, kama vile kilimo na miundombinu.

Ili kutimiza lengo la mabadiliko ya tabianchi lazima tutimize lengo la misitu:FAO/UNECE

Tabianchi na mazingira

Athari za mabadiliko ya tabia nchi kwenye misitu zitakuwa kubwa imesema ripoti iliyotolewa leo na shirikia la Umoja wa Mataifa la chakula na Kilimo FAO kwakushirikinana na kamisheni ya masuala ya uchumi barani ulaya UNECE. 

Ripoti hiyo” Utafiti wa mtazamo wa sekta ya misitu 2020-2040” imeeleza kuwa bado mifano ya kimataifa ya kupunguza uzalishaji wa gesi ukaa inategemea zaidi uwezo wa misitu kuchukua kaboni na kuongeza uzalishaji wa bidhaa mpya za kibunifu ambazo zinaweza kuchukua nafasi ya nyenzo zinazoingiza uzalishaji mkubwa zinazotumika katika ujenzi, nguo na uzalishaji wa nishati. 

Ripoti hiyo inawasilisha masuala ya kuzingatia katika sera yenye msingi wa kielelezo kwa tasnia ya misitu ili kusaidia minyororo ya ugavi endelevu na kuchangia katika juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi duniani na na kujenga mnepo. 

Matangazo yalitolewa katika mkutano wa COP26 kuhusu maendeleo madhubuti ya usimamizi na uhifadhi endelevu wa misitu.  

Viongozi 130, wanaowakilisha 90% ya misitu ya dunia, walitangaza kujitolea kusitisha na kuacha upotevu wa misitu na uharibifu wa ardhi ifikapo 2030.  

Kwa mujibu wa FAO “kufikia lengo hili hata hivyo ni kazi ngumu. Mikakati mbalimbali endelevu ya kukabiliana na upotevu wa misitu na kujenga mnepo inahitajika kwa kuzingatia muongo wa Umoja wa Mataifa wa marejesho ya mfumo wa ikolojia na malengo ya maendeleo endelevu, lakini pia lazima pia izingatie ongezeko la hatari ya matukio ya mabadiliko ya tabianchi kama vile milipuko ya wadudu, dhoruba, ukame na moto wa nyika.” 

Msitu katika ardhi ya Miguel Flores Pedraza, mkulima mzalishaji nchini Sierra Gorda, unakarabatiwa kwa ufadhili wa mradi wa Malipo kwa Huduma za Mazingira.
© Grupo Ecológico Sierra Gorda
Msitu katika ardhi ya Miguel Flores Pedraza, mkulima mzalishaji nchini Sierra Gorda, unakarabatiwa kwa ufadhili wa mradi wa Malipo kwa Huduma za Mazingira.

Mtazamo wa juhudi tofauti wahitajika 

Misitu katika eneo la UNECE inachangia asilimia 47% ya akiba ya hewa ukaa ya misitu duniani na hutoa 60% ya miti ya mbao inayotumiwa viwanda duniani, ambayo inaweza kutumika kuzalisha mazao endelevu ya misitu ili kusaidia mchakato wa kimataifa wa kuingia katika uchumi unaojali mazingira. Kudumisha uwiano kati ya uhifadhi na uzalishaji katika mazingira ya mabadiliko ya tabianchi kunahitaji mfumo wa sera kamilifu na endelevu. 

Utafiti huu unatoa uchanganuzi wa wazi, wenye lengo ili kusaidia nchi wanachama wa UNECE kukabiri biashara hizi huku ukiongeza uwezekano wa uvumbuzi na kutambua jukumu kuu ambalo misitu inachukua katika Nyanja ya kimataifa  kuhusu uzalishaji wa hewa ukaa. 

Bi. Olga Algayerova, katibu mtendaji wa UNECE, amesisitiza kuwa utafiti huu umefanyika katika wakati muhimu na muafaka “mahitaji ya kuni na mazao mengine ya misitu na huduma, ikiwa ni pamoja na uhifadhi wa bioanuwai na uvunaji wa hewa ukaa yanaongezeka na kubadilika. Matokeo yake, chaguzi zinazowakabili wasimamizi wa misitu na watunga sera zinakuwa ngumu zaidi. Utafiti wa mtazamo wa sekta ya misitu unaangazia masuala mchanganyiko ambayo yanahitaji kuzingatiwa kwa makini ili kuhakikisha kwamba mbinu endelevu za usimamizi wa misitu zinaendelea katika eneo la UNECE katika miongo ijayo." 

Naye Bwana. Vladimir Rakhmanin, mkurugenzi mkuu msaidizi wa FAO na Mwakilishi wa Kanda ya Ulaya na Asia ya Kati anakubaliana na Olga na kusema kwamba, "Matokeo ya utafiti wa mtazamo wa misitu yatasaidia kuimarisha juhudi za uzalishaji endelevu zaidi na biashara ya mazao ya misitu, ambayo ni muhimu katika kuendeleza maendeleo yaliyopatikana kuelekea ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu, kufikia malengo ya mkataba wa Paris na malengo ya maendeleo endelevu.”