Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
 Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina Mohammed akitoa hotuba yake katika uzinduzi wa Mpango wa kulinda mazingira wa Mashariki ya Kati nchini Saudi Arabia.

Hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi zinaweza kukuza utu, fursa na usawa: Mohammed

MGI Summit

Tabianchi na mazingira

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed ameshiriki katika majadiliano ya TED yanayosisitiza fursa za kuondokana na mgogoro wa mabadiliko ya tabianchi kwa kuchangisha fedha zaidi na mshikamano, wakati huu ambao "fursa bado ipo". 

Kwa mujibu wa Bi. Mohammed “Hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi zinaweza kuwa chombo cha kuchagiza utu, fursa na usawa kwa wote.” 

Amina Mohammed ameshiriki katika majadiliano hayo ya TED, na kusisitiza kwamba fedha zaidi na mshikamano ni viambato muhimu vya kutatua mgogoro wa sasa wa mabadiliko ya tabianchi. 

Mvuvi Falmata Mboh Ali (kulia) akiwa na mwenzake kwenye ziwa Chad wakisaka samaki ambao idadi yao imepungua kutokana na kusinyaa kwa ukubwa awa ziwa hilo.
UN News/Dan Dickinson
Mvuvi Falmata Mboh Ali (kulia) akiwa na mwenzake kwenye ziwa Chad wakisaka samaki ambao idadi yao imepungua kutokana na kusinyaa kwa ukubwa awa ziwa hilo.

Malengo ya maendeleo endelevu SDG’s 

Wakati dunia ikielekeza macho na masikio kwenye mkutano wa 26 wa Umoja wa Mataifa wa  wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP26, naibu mkuu wa shirika hilo anaialika kutafakari upya jinsi safari ya kutokomeza hewa ukaa itakavyokuwa , uwekezaji zaidi katika juhudi za mabadiliko ya tabianchi na, wakati huo huo, kuweka kipaumbele kwenye malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. 

Kiongozi huyo wa kundi la maendeleo endelevu la Umoja wa Mataifa pia anatetea kwamba sasa ni wakati wa "kupiga kelele kubwa ili kuubadilisha ulimwengu". 

Ukuta Mkuu wa Kijani wa Sahara na Mpango wa Sahel unasaidia jamii katika usimamizi endelevu wa maeneo kavu.
Photo: FAO/Giulio Napolitano
Ukuta Mkuu wa Kijani wa Sahara na Mpango wa Sahel unasaidia jamii katika usimamizi endelevu wa maeneo kavu.

Kabla ya kuteuliwa kuwa naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mohammed alikuwa waziri katika serikali ya Nigeria na alizungumzia maisha yake ya kupanda mlima kwenye bonde la ziwa Chad linalohusisha nchi za Chad, Cameroon, Niger na Nigeria, likiwaogesha watu milioni 30. 

Pia alizungumzia athari za mpango kabambe wa kupanda miti milioni 100 kwenye ukingo mkubwa wa mazingira uliopewa jina great Green Wall katika eneo la Sahel, kwa kupitia ufadhili zaidi wa kimataifa. 

Amesema miongoni mwa manufaa yangekuwa ni kuboreshwa kwa upatikanaji wa maji, matumizi ya ardhi, unafuu kutoka kwenye hali ya jangwa na kuimarika kwa uchumi wa kikanda unaojali mazingira kwa ajili ya watu nusu bilioni. 

Makubaliano 

Bi. Amina Mohammed amezitaka nchi kufikia makubaliano ya haraka kwenye mkutano wa COP26 mjini Glasgow na kutoa dola bilioni 100 ili kutimiza ahadi ya mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi, ahadi iliyoweka na nchi Tajiri kwa lengo la kuwasaidia walio na uhitaji zaidi. 

Bi. Mohammed amesema “Ingawa unaonekana kukosekana, kuna mshikamano ule ule ambao ulifikia kilele cha muafaka katika mkataba wa Paris na itifaki ya Montreal, tunashukuru jinsi tabaka la ozoni lilivyookolewa na ulimwengu unapona". 

Naibu mkuu wa Umoja wa Mataifa alitetea kwamba ari hii ya mshikamano inapaswa kurejewa upya mara moja, akionya kwamba "hatujachelewa lakini upenyo wa fursa unatoweka"

Naibu Katibu Mkuu, Amina J. Mohammed, akiwa ziaran nchini Mali alisafiri hadi Mopti, katikati mwa nchi hiyo ambako alitembelea mradi unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa wa "Femmes engagees".
MINUSMA/Harandane Dicko
Naibu Katibu Mkuu, Amina J. Mohammed, akiwa ziaran nchini Mali alisafiri hadi Mopti, katikati mwa nchi hiyo ambako alitembelea mradi unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa wa "Femmes engagees".

Matumaini kwa watu 

Amina Mohammed anasema ana matumaini kwa watu, ambao kupaza sauti zao kunasisitiza uharaka na kuinua sauti ya kwaya ya kimataifa ili viongozi wasiipuuze suala hili." 

Kuhusu msaada unaotolewa kwa hatua kali za mabadiliko ya tabianchi, amesisitiza kwamba umekuwa ukiongezeka, licha ya vikwazo, na kwamba lazima usisitishwe kwa sababu mabadiliko ya tabianchi yanaendelea.