Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Ripoti ya KM juu ya hali katika Sahara ya Magharibi

Ripoti ya KM, iliyowasilishwa wiki hii kuhusu hali katika Sahara ya Magharibi imependekeza Baraza la Usalama kutoa mwito kwa Morocco na Chama cha Ukombozi wa Sahara ya Magharibi, Frente Polisario, wa kuwahimiza kushirki kwenye majadiliano yasio na shuruti, ya kutafuta suluhu ya kuridhisha na ya kudumu, itakayowawezesha wazalendo wa Sahara ya Magharibi hatimaye kutekelezewa haki ya kujiamulia wenyewe utawala halali.

Matukio katika Sudan hivi sasa

Ofisi ya Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Kiutu (OHCHR) wiki hii imetoa mwito maalumu uitakayo Serekali ya Sudan kufanyisha uchunguzi huru juu ya mashambulio ya kikabila yaliyotukia kwenye eneo la Darfur hivi karibuni, ambapo inasemekena mamia ya raia waliuawa, na inadaiwa Serekali “ikijua juu ya tukio hili na baadhi ya wenye madaraka wanatuhumiwa hata kufadhilia zana za kuongoza jinai hiyo” dhidi ya raia.~

KM kuanzisha rasmi mfuko wa ujenzi wa amani

Ijumatano KM Kofi Annan alishiriki kwenye kikao maalumu cha kuanzisha Mfuko wa Ujenzi wa Amani wa UM utakaotumiwa kuyasaidia yale mataifa yanayoibuka kutoka hali ya uhasama kurudisha amani kwenye maeneo yao na kujiepusha na hatari ya kuteleza tena kwenye mapigano, vurugu na machafuko.

Hali ya usalama katika Darfur yazidi kuharibika

Shirika la UM juu ya Huduma za Amani katika Sudan (UNMIS) limeripoti kuwa hali ya usalama katika Darfur ya kusini, inaendelea kuharibika, hususan katika mji wa Gereida, kutokana na mvutano uliojiri na uhasama kati ya makabila yanoishi kwenye eneo hilo. Wakati huo huo kwenye mji wa Um al-Kher, Darfur ya Magharibi imeripotiwa kutukia vifo vya watu walioambukizwa na maradhi ya kipindupindu. Ripoti ya karibuni ya KM imeonya ya kuwayale mashirika yanayohudumia misaada ya kiutu huenda yakafunga operesheni zake pindi hali ya usalama haijadhibitiwa katika eneo kama ipasavyo. ~~