Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM apongeza maafikiano ya upatanishi katika Sudan

KM apongeza maafikiano ya upatanishi katika Sudan

KM ameripotiwa kuyapongeza yale maafikiano ya upatanishi yaliofikiwa karibuni kati ya Serekali ya Sudan na kundi la waasi wa Eneo la Mashariki. Mapatano haya yaliongozwa na Serekali ya Eritrea na kutiwa sahihi mjini Asmara tarehe 14 Oktoba.

KM alitumai mapatano haya yatasaidia kuimarisha amani kwenye eneo la mashariki ya Sudan na kurudisha utulivu katika sehemu zote za nchi. UM upo tayari kusaidia makundi husika, kwa kila njia, na kuhakikisha mapatano yao yatatekelezwa kama inavyotakiwa.