Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Vikosi vya MONUC kushiriki kwenye doria ya kuulinda mji mkuu wa Congo-DRC

Wanajeshi wa Shirika la UM juu ya Ulinzi wa Amani katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, yaani Shirka la MONUC wameanzisha, wiki hii, doria yenye mada isemayo “Kinshasa, mji usio silaha”, kwa makusudio ya kuzuia vikundi vyenye kuchukua silaha kutoaranda randa ovyo na kuzusha fujo na vurugu, hususan katika kipindi ambacho taifa linajiandaa kufanya duru ya pili ya uchaguzi wa raisi mwisho wa Oktoba. Vikosi vya MONUC vinashirikiana kwenye doria hii maalumu na majeshi ya taifa ya Congo-DRC pamoja na vikosi vya polisi vya kutoka Umoja wa Ulaya.

Uchaguzi wa KM mpya wa Umoja wa Mataifa unanyemelea

Ijumatatu tarehe 09 Oktoba (2006) Baraza la Usalama linatazamiwa kupiga kura ya kumteua rasmi KM mpya atakayechukua nafasi ya KM Kofi Annana mnamo mwanzo wa 2007. Baada ya hapo Baraza la Usalama litatuma jina la KM mpya mbele ya Baraza Kuu kuidhinishwa na wawakilishi wa kimataifa.

WHO yahimiza huduma za usafi wa hewa katika miji

Shirika la Afya Duniani (WHO) limependekeza serekali zote za kimataifa kuongeza huduma zao katika kuboresha usafi wa hewa katika miji yao. WHO ilisema pindi hatua hii itachukuliwa na miji husika itasaidia kuhifadhi afya na maisha ya watu milioni 2 ambao hufariki kila mwaka duniani kutokana na uharibifu wa hewa.~~

Juhudi za kupunguza umasikini katika nchi zenye uchumi mdogo (Sehemu ya Pili)

Hivi karibuni wajumbe wa kimataifa walikusanyika kwenye Makao Makuu ya UM, mjini New York, kuhudhuria Mkutano Mkuu maalumu wa Baraza Kuu, uliofanya mapitio juu ya utekelezaji wa ule Mpango wa Utendaji wa Brussels wa 2001. Mkutano huo wa Daraja ya Juu ulisailia juhudi za kuimarisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika yale mataifa 50 yenye uchumi wa kima cha chini kabisa, mataifa ambayo hujulikana kama LDCs.~~