Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utumiaji mabavu katika Liberia dhidi ya watoto na wanawake wautia wasiwasi UM

Utumiaji mabavu katika Liberia dhidi ya watoto na wanawake wautia wasiwasi UM

Ripoti ya tano juu ya haki za kiutu ya Shirika la Ulinzi wa Amani katika Liberia (UNMIL) imeonya ya kuwa makosa ya jinai ya kijinsia, ya kutumia nguvu na mabavu dhidi ya wanawake na watoto wadogo bado yanaendelea kuendelezwa katika Liberia.