Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matukio katika Sudan hivi sasa

Matukio katika Sudan hivi sasa

Ofisi ya Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Kiutu (OHCHR) wiki hii imetoa mwito maalumu uitakayo Serekali ya Sudan kufanyisha uchunguzi huru juu ya mashambulio ya kikabila yaliyotukia kwenye eneo la Darfur hivi karibuni, ambapo inasemekena mamia ya raia waliuawa, na inadaiwa Serekali “ikijua juu ya tukio hili na baadhi ya wenye madaraka wanatuhumiwa hata kufadhilia zana za kuongoza jinai hiyo” dhidi ya raia.~

•Halkadhalika, Ofisi ya OHCHR imependekeza kwa Serekali ya Sudan isaidie kurahisisha ugawaji wa misaada ya kiutu na madawa kwa wale wahamiaji wa ndani ya nchi waliopo kwenye kambi mbali na makwao, na kuhakikisha maeneo hayo yanapatiwa ulinzi imara unaoaminika.

•Tume ya wataalamu wanaosimamia utekelezaji wa vikwazo vya silaha katika Sudan wameripoti kutukia uharamishaji wa hali ya wa vikwazo hivyo unaofanyika bila ya kificho na makundi yote husika, ikijumuisha vikosi vya Serekali, wanamgambo wenzi wa Janjaweed, vikundi vya waasi wa kizalendo na pia wale waasi waliotokea taifa jirani la Chad, ambao ndio kundi halisi lenye kuchochea mzozo wa Darfur.