Mpango wa Utendaji wa UM Kudhibiti Silaha Ndogo Ndogo Wafanyiwa Mapitio
Miaka mitano baada ya Umoja wa Mataifa (UM) kupitisha Mpango wa Utendaji wa kukabiliana na biashara haramu ya silaha ndogo ndogo na silaha nyepesi katika dunia, Makao Makuu ya UM yalishuhudia mkusanyiko wa hali ya juu wa wawakilishi karibu 2,000 wa kimataifa kutoka serikali wanachama mbalimbali, pamoja na mashirika ya kikanda na kimataifa kwa makusudio ya kuzingatia uwezekano wa kulikomesha tatizo la kuenea kwa silaha ndogo ndogo na silaha nyepesi katika ulimwengu.