Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti kuhusu tatizo la utumiaji nguvu dhidi ya wanawake

Ripoti kuhusu tatizo la utumiaji nguvu dhidi ya wanawake

Mapema wiki hii, KM Kofi Annan aliwasilisha mbele ya Kamati ya Tatu ya Baraza Kuu, ambayo inahusika na masuala ya kijamii, kiutu na kitamaduni, ripoti maalumu inayozingatia tatizo sugu, na karaha, la utumiaji nguvu dhidi ya wanawake.

Rachel Mayanja, ni Mshauri Maalumu wa KM juu ya Masuala ya Jinsia na Maendeleo ya Wanawake na anatuchambulia kwenye kipindi umuhimu wa ripoti ya KM katika hekaheka za kutafuta suluhu ya kuridhisha itakayowavua wanawake na mateso ya kunyanyaswa na utumiaji wa mabavu dhidi yao.

Sikiliza taarifa kamili kwenye redio ya mtandao.