Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM yashiriki kikamilifu kuhudumia umma muathiriwa na mafuriko Afrika Mashariki

UM yashiriki kikamilifu kuhudumia umma muathiriwa na mafuriko Afrika Mashariki

Hivi majuzi, Afrika Mashariki ilikabiliwa na tatizo la mafuriko ya kihistoria yaliotukia baada ya mvua kali kunyesha mwisho wa mwaka 2006. Maafa haya yalisababisha uharibifu mkubwa wa hali na mali, hususan, miongoni mwa wale wahamiaji waliopo mipakani kati ya Kenya na Usomali.

Tunazingatia mchango wa UM kuhudumia kihali umma ulioathirika na mafuriko katika Afrika Mashariki. Kadhalika tuna ripoti ya mwandishi habari wa Redio ya UM juu ya huduma za WFP nchini Kenya. Sikiliza taarifa kamili kwenye idhaa ya mtandao.