Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kumbukumbu za miaka 10 ya uongozi wa KM mstaafu Kofi Annan katika UM (Sehemu ya Kwanza)

Kumbukumbu za miaka 10 ya uongozi wa KM mstaafu Kofi Annan katika UM (Sehemu ya Kwanza)

KM mstaafu Kofi Annan, siku chache kabla ya kumaliza uongozi wake wa miaka 10 katika Umoja wa Mataifa, aliitisha kikao cha mwisho cha mahojiano na waandishi habari wa kimataifa waliopo Makao Makuu mjini New York. Alizungumzia masuala mbalimbali na kuchambua taratibu zinazohitajika kutekelezwa ili kuboresha uhusiano wa kimataifa miongoni mwa Mataifa Wanachama.

Katika sehemu hii ya kwanza ya mfululizo wa makala mbili, KM Annan anazingatia masuala yanayohusu maendeleo, kwa ujumla, katika Afrika. Sikiliza taarifa kamili kwenye idhaa ya mtandao.