Sudan Kusini hawaombi mambo mengi isipokuwa usalama wa familia zao-Balozi Craft
Mwakilishi wa kudumu wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Balozi Kelly Craft amezuru mji wa Malakal nchini Sudan Kusini ambako amekutana na wanawake kutoka katika maeneo ya ulinzi wa raia na pia akatembelea kituo cha kuzalisha maji cha shirika la World Vision ambacho kinasaidia kupunguza uhaba wa maji safi na ya kunywa.