Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Sudan Kusini

Kijiji nchini Sudan Kusini, barabarani kati ya Yambio na Maridi, Equatoria ya Magharibi.
UN Photo/JC McIlwaine

Filamu yatumika kupambana na ndoa za utotoni na ukatili mwingine wa kingono Sudan Kusini 

Filamu mpya iliyopewa jina, “Zuia ndoa za utotoni Sudan Kusini” imeoneshwa kwa mara ya kwanza kwa wanajamii katika eneo la Yambio jimboni Equatoria Magharibi ikiwa na lengo la kupambana na unyanyasaji wa kingono unaohusiana na migogoro pamoja na ubakaji ambavyo ni matukio ya kawaida katika nchi hiyo changa zaidi ulimwenguni.  

Sauti
3'7"
Walinda amani wa Ethiopia wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko Sudan Kusini (UNMISS) wakisindikiza kikundi cha wanawake nje ya eneo linalosimamiwa na Umoja wa Mataifa na hivyo kuwawekea mazingira salama ambapo wanaweza kutafuta kuni bila kuwa katika hatari
UNMISS\Nektarios Markogiannis

UNMISS yatoa mafunzo kwa jeshi la Sudan Kusini kuzuia ukatili wa kingono 

Ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa malengo ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake  miaka 75 ya uwepo wake,  kuwa mtetezi mkubwa wa amani na haki za wanadamu kote duniani, nchini Sudan Kusini, mpango wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini, UNMISS umeshirikiana na Jeshi la wananchi wa Sudan Kusini SSPDF kuwapa mafunzo wakufunzi kuhusu kuzuia ukatili wa kingono unaohusiana na mizozo.

Sauti
2'41"
Familia iliyotawanywa ikiondoka katika kambi ya ulinzi wa raia ya Umoja wa Mataifa mjini Juba kurejea nyumbani kwao Jonglei Sudan Kusini
UN Photo/Isaac Billy

Njaa inatumiwa kama mbinu ya vita huko Sudan Kusini - Jopo la UN 

Ripoti yenye kurasa 46 iliyotolewa leo mjini Geneva Uswisi na tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNCHRSS, imeeleza kuwa Sudan Kusini tangu ilipopata uhuru wake mwaka 2013, mzozo wa kikatili nchini humo umesababisha mateso yasiyoweza yasiyopimika kwa raia na kusababisha kiwango viwango vya kutisha vya ukosefu wa chakula na utapiamlo hali ambayo inatumiwa kama mbinu ya vita.