Malori ya UN yasipoachiliwa, huduma za kiutu Sudan Kusini zitakwama- Haysom
Kufuatia tamko la serikali ya Sudan Kusini la kufuta uamuzi wake wa awali wa kutoza kodi malori yenye shehena za mafuta, Umoja wa Mataifa nchini humo umesihi kuachiliwa haraka kwa malori yake yaliyosheheni bidhaa hiyo pamoja na vifaa vingine muhimu.