Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sudan Kusini

Mtoto mwenye umri wa mwaka 1 anafanyiwa unchunguzi wa matibabu kama kuna dalili za utapiamlo katika kituo cha mapokezi kwenye mpaka wa Sudan na Sudan Kusini.
© WFP/Hugh Rutherford

Uongozi wa jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini waomba usaidizi zaidi wa ulinzi

Huku mzozo wa Sudan ukiendelea, wakimbizi na wanaorejea wanamiminika katika mipaka ya nchi jirani ya Sudan Kusini, wengi wamekuwa wakitafuta hifadhi katika jimbo la Upper Nile nchini humo na wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu.  Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS umefanya mazungumzo na uongozi wa jimbo hilo kuona namna ya kuwasaidia.

Sauti
2'25"
Familia ya wakimbizi wa Sudan Kusini wanaorejea wakisubiri katika kituo cha UNHCR cha Renk, Sudan Kusini. (Maktaba)
© UNHCR/Andrew McConnell

UNHCR na Benki ya Maendeleo ya Afrika waungana kusaidia wakimbizi nchini Sudan Kusini

Vita vinapotokea wananchi wanalazimika kusaka kila namna ya kujilinda na kuokoa maisha yao. Mambo yanapokuwa mabaya watu hao hulazimika kuacha kila kitu nyuma na kukimbia kwenda kusaka hifadhi sehemu nyingine. Watu hao wanapoondoka wanaondoka na ujuzi wao mfano kama alikuwa muuguzi, mfanya biashara, fundi muashi au taaluma yoyote ile. 

Sauti
3'47"
Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS), Nicholas Haysom akihutubia waandishi wa habari jijini Juba kuhusu hali ya usalama nchini Sudan Kusini.
UNMISS/Gregório Cunha

Sudan Kusini: Hatua inahitajika sasa kwa ajili ya uchaguzi kwa wakati na wa huru na haki - Nicholas Haysom  Haysom

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS), Nicholas Haysom ametahadharisha kwamba muda unazidi kuyoyoma kuelekea Sudan Kusini kufanya uchaguzi mkuu unaotarajiwa mwezi Desemba mwaka ujao wa 2024 lakini bado masuala muhimu ya kuufanya uchaguzi huo uende kama ulivyopangwa bila kuchelewa hayajakamilika.

Sauti
2'18"
Nyumba ya familia huko Terekeka, Sudan Kusini.
Picha: FAO/Albert González Farran

FAO yasaidia jamii ya Wavuvi Sudan Kusini kutengeneza mnyororo wa thamani

Mkuu wa Mpango wa umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini UNMISS ambaye pia ni mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo Nicholas Haysom amefanya ziara maalum ya kutembelea visiwa vilivyopo katika kaunti ya Terekeka na kujionea utekelezaji wa miradi ya stadi za maisha inayoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO. 

Sauti
3'3"
Wananchi wa Sudan Kusini washerehekea tamasha la utamaduni la amani katika mji wa Aweil.
UNMISS

Tamasha la utamaduni wa amani layaleta pamoja makabila ya Sudan Kusini

Mwanzoni mwa mwezi huu wa April dunia iliadhimisha Siku ya Kimataifa ya michezo kwa maendeo na amani, nchini Sudan Kusini kwa siku mbili mfululizo maelfu ya wananchi wa walikusanyika kusherehekea tamasha la utamaduni la amani lililoandaliwa na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS kwa kushirikiana na Wizara ya Utamaduni ya jimbo la Kaskazini la Bahr El Ghazal.

Sauti
4'27"