Ulemavu hautuzuii kubadili maisha yetu
Dhana potofu kuwa ulemavu ndio ukomo wa maisha imetupiliwa mbali huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Wakimbizi wa kike na wa kiume kutoka Burundi wamechukua hatua.
Dhana potofu kuwa ulemavu ndio ukomo wa maisha imetupiliwa mbali huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Wakimbizi wa kike na wa kiume kutoka Burundi wamechukua hatua.
“Ni muhimu pande zote hususan serikali itangaze ahadi yake kwenye mchakato unaoongozwa na Jumuiya Afrika Mashariki, na kufikia makubaliano kabla ya uchaguzi mkuu mwaka 2020”
Idadi kubwa ya wakimbizi wa Burundi wanahofiwa kufariki dunia baada ya mabasi walimokuwa wakisafiria kurejea nyumbani kutoka Tanzania kupata ajali mkoani Kagera, kaskazini-magharibi mwa Tanzania.
Haki za binadamu zinazidi kusiginwa maeneo mbalimbali duniani hata katika nchi ambazo kwa muda mrefu zimetambuliwa kuwa visiwa vya amani, asema Zeid Ra'ad Al Hussein hii leo katika ripoti yake kuhusu hali ya haki za binadadamu duniani.
Rais wa baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa, balozi Vojislav Suc amemteua Lucy Asagbor kutoka Cameroon kuwa mjumbe wa kamati ya tume ya uchunguzi kuhusu Burundi.
Nchini Burundi, sintofahamu ya kisiasa, kiuchumi na kijamii iliyoanza baada ya Rais Pierre Nkurunzinza kuongeza muda wa uongozi na kuingia awamu ya tatu bado inaendelea na sasa yaelezwa kuwa shughuli za vyama vya kisiasa zinaendeshwa na watu wachache.
Zaidi ya wakimbizi 400,000 wa Burundi waliokimbia machafuko na kutokuwepo usalama nchini mwao sasa, wanahitaji msaada wa haraka na ukata unatishia mustakhbali wao, limeonya leo shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. Siraj Kalyango na tarifa kamili
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linasema haba na haba hujaza kibaba kwa wakimbizi, hususani ambao sasa wamepata maskani ya kudumua na kuanza kujenga upya maisha yao kama binti sandrine kutoka Burundi.Siraj Kalyango anatupasha zaidi
Kampeni kuhakikisha kwamba ukatili dhidi ya wanawake na wasichana zinashika kasi kila uchao katika zama hizi ambazo Umoja wa Mataifa na wadau wake wanataka kuona vitendo hivyo dhalimu vinatokomezwa.
Televisheni au kwingineko ikijulikana kama Runinga imeleta mabadiliko makubwa katika mtazamo wa vipindi hususan kwenye nchi ambazo awali radio ilikuwa imeshika kasi. Televisheni ina umuhimu wake katika kuhabarisha, kuelimisha na hata kuburudisha na ndio maana tarehe 21 ya mwezi Novemba imetengwa kuwa siku ya televisheni duniani.