Kamati ya UN yatiwa hofu na visa vya utesaji watu Burundi, yataka serikali ichukue hatua
Kamati ya Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu dhidi ya Utesaji, CAT imetamatisha kikao chake cha 78 huko Geneva, Uswisi kwa kuto hitimisho za ripoti za mataifa 6 ikiwemo Burundi ambapo inaonesha wasiwasi juu ya utekelezaji wa Mkataba wa Kimataifa dhidi ya Mateso na adhabu za kikatili zisizoheshimu utu.