Ukata wakwamisha mipango ya kusaidia wakimbizi Tanzania
Nchini Tanzania harakati za serikali kusaidia wakimbizi ikiwemo hata kuwapatia uraia baadhi yao waliokidhi vigezo bado zinahitaji kuungwa mkono na mashirika mengine ili ziweze kusonga mbele zaidi kwa kuwapatia raia hao wapya misaada mingine ya kukidhi mahitaij yao.