Zahma ya wakimbizi wa Burundi yaelekea kusahaulika:UNHCR

6 Februari 2018

Zaidi ya wakimbizi 400,000 wa Burundi waliokimbia machafuko na kutokuwepo usalama nchini mwao sasa, wanahitaji msaada wa haraka na ukata unatishia mustakhbali wao, limeonya leo shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. Siraj Kalyango na tarifa kamili

UNHCR na wadau wake hivi sasa wanahaha kutoa msaada na ulinzi kwa wakimbizi hao ambao wengi wapo Tanzania, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Uganda na nchi zingine za jirani.

Na ufadhili finyu unamaanisha wakimbizi hawa hawataweza kuishi tena kwa usalama na utu wanaohitaji na kustahili. Hali katika kambi za muda inazidi kuzorota huku kambi za kudumu zikifurika kupita kiasi mfano kambi ya Mahama nchini Rwanda. Janet Pima ni afisa ulinzi wa UNHCR kambini hapo

(SAUTI YA JANET PIMA)

“Hivi sasa kambi imefurika, tuna takribani wakimbizi 54,000 kambini na nafasi tuliyonayo yote imeshachukuliwa na kambi za muda na hatuna nafasi tena na hiyo ni changamoto kubwa tuliyonayo sasa.”

Hivi sasa kambi imefurika, tuna takribani wakimbizi 54,000 kambini na nafasi tuliyonayo yote imeshachukuliwa na makambi ya muda na hatuna nafasi tena na hiyo ni changamoto kubwa tuliyonayo sasa.”

UNHCR,na washirika wengine 26 wa misaada ya kibinadamu leo wamezindua ombi la dola milioni 391 ili kukidhi mahitaji ya muhimu ya wakimbizi wa Burundi 430,000 kwa mwaka 2018. 

Changamoto zinazowakambili wakimbizi hao kwa mujibu wa UNHCR ni lukuki na hali inakuwa mbaya zaidi kwa wale wenye mahitaji maalumu kama Dorothe Nahayo mlemavu anayeishi na wanawe  watatu kwenye kambi ya Lusenda nchini DRC

(SAUTI YA DOROTHE NAHAYO) 

UNHCR imeongeza kuwa fedha hizo zisipopatikana basi zahma ya Burundi itakuwa imesahaulika pamoja na wakimbizi wanaohusika.

 

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter