Mjumbe mwingine ataeuliwa katika tume ya haki kuhusu Burundi

5 Machi 2018

Rais wa baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa, balozi Vojislav Suc amemteua  Lucy Asagbor kutoka Cameroon kuwa mjumbe wa kamati ya tume ya uchunguzi kuhusu Burundi.

Bi Asuagbor anachukua nafasi ya Reina Alapini Gansu kutoka Benin ambae amekuwa katika tume hiyo tangu Novemba mwaka 2016 na majuzi alitangaza kung’atuka kutoka nafasi hiyo baada ya kuchaguliwa  kama jaji wa mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai ICC ya mjini The Hague.

Bi Asuagbor amefanya kazi katika idara ya mahakama kwa kipindi cha miaka 30, kama jaji  wa mahakama kuu na rais wa kitengo cha uchunguzi cha mahakama kuu ya Cameroon.

Makamishna wa tume hiyo , wanawajibika kuchunguza ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Burundi uliofanyika tangu April 2015 katika juhudi za kukabiliana na tabia ya kutohofia kuchukuliwa hatua za kinidhamu na pia kuwatambua wanaodaiwa  kuhusika na visa kama hivyo kwa lengo la kuwawajibisha.

Tume hiyo itatoa tarifa ya maendeleo ya kina ya shughuli zake kwa baraza  baraza la haki za binadamu mnamo Machi 13.

 

 

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud