Burundi: Mbinu ya mashangazi na mababa wa shuleni yaepusha watoto wakimbizi dhidi ya kejeli kutoka kwa wenzao
Nchini Burundi shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limechukua hatua kuhakikisha watoto wakimbizi wanaorejea nchini humo wanaweza kuendelea na elimu bila uoga na jakamoyo hasa pale wanapokumbana na vizuizi vya tofauti ya lugha waliyotumia ukimbizini na ile inayotumika nyumbani walikorejea.