Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukatili dhidi ya wanawake marufuku Burundi: Seruka

Kampeni za shirika lisilo la kiserikali la SERUKA kwenye uwanja wa Parke mjini Bujumbura. Picha: UM/ Ramadhan Kibuga

Ukatili dhidi ya wanawake marufuku Burundi: Seruka

Wanawake

Kampeni kuhakikisha kwamba ukatili dhidi ya wanawake na wasichana zinashika kasi kila uchao katika zama hizi ambazo Umoja wa Mataifa na wadau wake wanataka kuona vitendo hivyo dhalimu vinatokomezwa.

Ukatili wa kijinsia ni changamoto kubwa nchini Burundi huku Zaidi ya asilimia 90 ya wanaotendewa ukatili huo wakiwa ni wanawake na watoto. Sasa shirika lisilo la kiserikali la SERUKA limeamua kushikia bango dhuluma hiyo kwa kuendesha kampeni katika maeneo mbalimbali nchini humo kupinga na kuelimisha jamii kuachana na ukatili dhidi ya wanawake. Mwandishi wetu wa maziwa makuu Ramadhan Kibuga alitembelea moja ya kampeni za shirika hilo kwenye uwanja wa Parke mjini Bujumbura uangana naye kwenye Makala hii.