Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umuhimu wa televisheni ni zaidi ya kuhabarisha nchini Burundi

Umuhimu wa televisheni ni zaidi ya kuhabarisha nchini Burundi

Utamaduni na Elimu

Televisheni au kwingineko ikijulikana kama Runinga imeleta mabadiliko makubwa katika mtazamo wa vipindi hususan kwenye nchi ambazo awali radio ilikuwa imeshika kasi. Televisheni ina umuhimu wake katika kuhabarisha, kuelimisha na hata kuburudisha na ndio maana tarehe 21 ya mwezi Novemba imetengwa kuwa siku ya televisheni duniani.

Hata hivyo maadhimisho ya nyakati hizo yanakuja na mengi zaidi wakati huu ambapo nchi zinazoendelea zikiwa katika utaratibu wa kuondoka kwenye mfumo wa zamani wa Analogia na kuingia mfumo mpya wa dijitali.Mageuzi  haya yanafanyika wakati ni idadi ndogo sana ya wananchi wenye kumiliki au kupata fursa ya kuona Televisheni.

Isitoshe Televisheni  katika nchi masikini zinakumbwa na  changamoto ya ukosefu mkubwa  wa vifaa. Je hali ikoje ya matumizi ya teknolojia hiyo na changamoto ni zipi? Mwandishi wetu wa Maziwa Makuu Ramadhani Kibuga amejikita huko Bujumbura, Burundikwenye televisheni ya Taifa na ungana naye kwenye makala haya.

(MAKALA YA KIBUGA)