Njia ya kupitisha mkataba mpya wa wahamiaji sasa ni ‘nyeupe’- UNHCR
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema sasa kuna matumaini makubwa ya kupitishwa kwa mkataba wa kimataifa kuhusu wakimbiz na wahamiaji, GCM mwezi ujao.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema sasa kuna matumaini makubwa ya kupitishwa kwa mkataba wa kimataifa kuhusu wakimbiz na wahamiaji, GCM mwezi ujao.
Katika kipindi cha zaidi ya muongo mmoja waandishi habari takriban elfu moja wameuawa wakati wanafanya kazi yao adhimu, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika ujumbe wake wa siku ya kimataifa ya kukomesha ukwepaji sheria kwa uhalifu dhidi ya waandishi wa habari.
Rais wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC Jaji Chile Eboe-Osuji amesema ushirikiano wa kimataifa ndio nguzo pekee ya kuendeleza kazi za mahakama hiyo iliyoanzishwa miaka 20 iliyopita.
Hivi karibuni katika mlolongo wa mijadala ya Afrika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kulifanyika mkutano wa siku moja kuhusu jinsi jamii ya kimataifa inaweza kukomesha milio ya bunduki barani Afrika, mkutano ambao ulihudhuriwa na wawakilishi wa nchi wanachama wakiwemo wabunge.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake, UN-Women, Phumzile Mlambo-Ngucka ametaka jamii ya kimataifa iachane na harakati za juujuu zisizoweza kuleta matunda katika kujumuisha wanawake kwenye ulinzi na amani duniani.
"Taarifa ya jana ya Balozi wa Burundi kwenye Umoja wa Mataifa Albert Shingiro kushambulia ripoti ya tume huru ya kimataifa ya Uchunguzi iliyoanzishwa na Baraza la Haki za binadamu la Umoja wa Mataifa inasikitisha na kwa mada na sauti iliyotumika."
Leo ni siku ya Umoja wa Mataifa ikiwa ni maadhimisho yanayolenga kusherehekea kuanza kutumika kwa katiba ya chombo hicho tarehe 24 Oktoba mwaka 1945.
Sasa imethibitishwa kuwa wanamichezo wakimbizi watashiriki katika mashindano ya olimpiki huko Tokyo Japan mwaka 2020.
Fedha za ufadhili kwa mamilioni ya watu waliolazimika kukimbia makwao na wasio na utaifa zinazidi kuwa finyu na kuwaacha watu hao wakibeba gharama kubwa ya kutotimiziwa mahitaji yao ya msingi. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa leo na kitengo cha wahisani na huduma ya kukusanya fedha cha shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR.
Waziri wa mambo ya nje wa Burundi amesema kwa ujumla hali ya usalama na utulivu imerejea Burundi na kilichosalia ni matukio madogomadogo ya utovu wa nidhamu.