Kutoka Tanzania hadi Makamba nchini Burundi- Asante UNHCR na wadau
Akiwa katika ziara yake ya kwanza nchini Burundi hivi karibuni, Naibu Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi duniani, UNHFR Kelly Clements ameisihi jamii ya kimataifa iongeze msaada kwa maeneo na jamii ambako wakimbizi wa Burundi wameamua kurejea nyumbani kwa hiari.