Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haba na haba hujaza kibaba kwa wakimbizi:UNHCR

Wakimbizi kutoka Burundi.
PICHA: UNHCR/Maktaba/Eduardo Soteras Jalil
Wakimbizi kutoka Burundi.

Haba na haba hujaza kibaba kwa wakimbizi:UNHCR

Wahamiaji na Wakimbizi

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linasema haba na haba hujaza kibaba kwa wakimbizi, hususani ambao sasa wamepata maskani ya kudumua na kuanza kujenga upya maisha yao kama binti sandrine kutoka Burundi.Siraj Kalyango anatupasha zaidi

Ni sauti ya Sandrine akisema anajivunia ujuzi alioupata, sasa anaweza kushona nguo kama fundi cherahani. Ni binti wa miaka 18 alikimbia machafuko Burundi na sasa maskani yake ni nchini Rwanda kama mkimbizi.

Anasema kilichomfanya kukimbia ni kuokoa maisha yake, hivi sasa akiwa salama katika kambi ya wakimbizi ya Mahama anajifunza ufundi cherahani katika kituo cha wanawake kupitia mradi unaofadhiliwa na shirika la UNHCR. Sandrine anaeleza kwa nini alijiunga na mradi huo

(Sauti ya Sandrine)

“Moja ya sababu zilizonileta hapa ni kujifunza ujuzi wa kushona ambao utanisaidia kupata fedha ili niweze kusaidia familia yangu.”

 Mbali ya ushonaji wanawake kituoni hapo wanajifunza pia kuendesha biashara. Na kwa ujuzi alioupata Sandrine anataka kusaidia wanwake wengine

(Sauti ya Sandrine)

“Endapo nitarudi Burundi siku moja , nitakuwa fundi cherahani na kuwasaidia wanawake na wasichana wengine , na kuwafundisha kushona.”

UNHCR imekuwa ikisaidia mamilioni ya wakimbizi kama Sandrine kuanza kujenga upya Maisha yao baada ya kupama mahala salama pa kuishi.