Ulemavu hautuzuii kubadili maisha yetu

17 Aprili 2018

Dhana potofu kuwa ulemavu ndio ukomo wa maisha imetupiliwa mbali huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Wakimbizi wa kike na wa kiume kutoka Burundi wamechukua hatua.

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, wakimbizi kutoka Burundi ambao waliamini kuwa maisha yao yatazidi kuwa duni kutokana na ulemavu, sasa nuru imeanza kuwaangazia baada ya kutumia stadi na maarifa yao kuboresha maisha. Taarifa zaidi na John Kibego

Katika kambi ya wakimbizi ya Lusenda, jimboni Kivu Kusini nchini DRC,  wakimbizi 32 wanawake na wanaume kutoka Burundi ambao wote wana ulemavu wamechukua hatua ya kijasiri.

Wamepuuza fikra potofu ya kwamba ulemavu ni kukosa uwezo. Miongoni mwao ni Mathias Nzorigendera ambaye ubaguzi uliwapa machungu.

(Sauti ya Mathias Nzorigendera)

UNICEF/Sebastian Rich
Kuwa na ulemavu siyo ukomo wa maisha.

Na ndipo wakachukua hatua ya kuunda kikundi kiitwacho Dufashanye yaani tusaidiane kwa kirundi na kufungua karakana ya kutumia vyuma chakavu kutengeneza sufuria, sahani, birika na pasi za mkaa.

(Sauti ya Mathias Nzorigendera)

Vyombo  hivyo vinauzwa kwenye soko lililopo kambini Lusenda. Pamoja na kupata usaidizi kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, Dufashanye wana ndoto zaidi.

(Sauti ya Mathias Nzorigendera)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud