Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wa mitungi ya gesi kwenye kambi za wakimbizi Tanzania ni mkombozi wa wanawake

Wakimbizi kutoka Burundi wakipika chakula kutumia kuni
UNICEF/Seck
Wakimbizi kutoka Burundi wakipika chakula kutumia kuni

Mradi wa mitungi ya gesi kwenye kambi za wakimbizi Tanzania ni mkombozi wa wanawake

Wahamiaji na Wakimbizi

Tatizo la ukosefu wa nishati endelevu kwa ajili ya kupikia, limekuwa kikwazo kikubwa kwa jamii ya wakimbizi nchini Tanzania, ambako wanawake na wasichana wamekuwa wakikabiliwa na ubakaji pindi wanapoenda kuokota kuni.

Miongoni mwao ni Frida Nehebauwayo msichana mkimbizi kutoka Burundi mwenye umri wa miaka 17 ambaye amesema pamoja na vitendo vya ukatili hukosamasomo kwa kuwa kazi ha kuchanja kuni huanza saa 12 asubuhi.

Amesema, jambo hilo linahatarisha mustakabali wa maisha ya wasichana wengi katika kambi za wakimbizi.

Hata hivyo nuru imeingia kwa kuwa Mradi wa nishati ya gesi , ulioanzishwa na shirika la Umoja wa Mataifa kuhudumia wakimbizi UNHCR, umekuwa si tu mkombozi kwa wakimbizi wanawake na wasichsna bali pia kwa uhifadhi wa misitu nchini Tanzania na pia upunguzaji wa kaboni katika uchafuzi wa mazingira.

UNHCR imesema, kuanzishwa kwa mradi huu kumesaidia kupunguza matumizi ya kuni kutoka asilimia 92 hadi 30, jambo ambalo litaokoa maisha ya maelfu ya wanawake na wasichana.

Frida anasema kwakeyeyeni habari njema kwani anapata muda wa kuhuduria vipindi vya asubuhi shuleni kwake.

UNHCR, pamoja na washirika wake zikiwemo kampuni za kuzalisha nishati ya gesi nchini Tanzania wanasema wataendelea kujitolea kadri ya uwezo wao kama mojawapo za fursa za kuimarisha ulinzi na usalama kwa wanawake na wasichana katika kambi za wakimbizi.