Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukata wakwamisha mipango ya kusaidia wakimbizi Tanzania

Mawio kambini Nduta mkoani Kigoma nchini Tanzania ambako ni makazi ay wakimbizi kutoka Burundi.
UNHCR/Sebastian Rich
Mawio kambini Nduta mkoani Kigoma nchini Tanzania ambako ni makazi ay wakimbizi kutoka Burundi.

Ukata wakwamisha mipango ya kusaidia wakimbizi Tanzania

Wahamiaji na Wakimbizi

Nchini Tanzania harakati za serikali kusaidia wakimbizi ikiwemo hata kuwapatia uraia baadhi  yao waliokidhi vigezo bado zinahitaji kuungwa mkono na mashirika mengine ili ziweze kusonga mbele zaidi kwa kuwapatia raia hao wapya misaada mingine ya kukidhi mahitaij yao.

Tanzania imesihi Umoja wa Mataifa na jumuiya ya kimataifa iongeze usaidizi wake kwa shirika la kuhudumia wakimbizi duniani, UNHCR ili hatimaye liweze kufanikisha operesheni zake za kusaidia wakimbizi waliosaka hifadhi nchini humo.

Akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani hivi karibuni, Mkuu wa Idara ya uhusiano wa kimataifa kwenye Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania Balozi Celestine Mushi amesema ukosefu wa fedha unakwamisha operesheni hizo na kwamb..

(Sauti ya Balozi Celestine Mushi)

Kwa mantiki hiyo amesema..

(Sauti ya Balozi Celestine Mushi)

Tanzania inahifadhi zaidi ya wakimbizi 350,000 kutoka nchi kadhaa ikiwemo Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na Sudan.

TAGS: Tanzania, wakimbizi, UNHCR,