Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Je wasaidia vipi wakimbizi hapo ulipo?

Wakimbizi kutoka nchi tofouti wanaosaka hifadhi nchini Sweden wacheza muziki katika tamasha la muziki lililoandaliwa na UNHCR na El Sistema huko Sergels Torg in Stockholm
UNHCR/Caroline Bach
Wakimbizi kutoka nchi tofouti wanaosaka hifadhi nchini Sweden wacheza muziki katika tamasha la muziki lililoandaliwa na UNHCR na El Sistema huko Sergels Torg in Stockholm

Je wasaidia vipi wakimbizi hapo ulipo?

Wahamiaji na Wakimbizi

Huu ndio wakati wa ulimwengu kujitokeza kusaidia wale wote waliolazimishwa kukimbia makazi yao kutokana na sababu zisizoepukika.

Wito huo umetolewa na mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya jamii za watu wachache , Fernand de Varennes, kupitia taarifa yake  ya kuadhimisha siku ya wakimbizi duniani.

Amemtaka kila mtu kuunga mkono hatua za kusaidia wakimbizi kama vile kuwapatia elimu, makazi na mafunzo ya kuwawezesha kufanya kazi.

Amesema kuwa kila dakika, watu 20 kutoka maeneo tofauti kijiografia, kikabila, kidini ama kirangi, wanalazimishwa  kuacha makazi yao kutokana na chuki au migogoro, wengi wao wakitoka katika jamii za wachache na wanaotengwa.

Ameongeza kuwa katika siku hii ambayo jamii ya kimataifa inamulika masuala ya utu, nguvu pamoja na ujasiri wa wakimbizi licha ya madhila, ni vyema kufanya kila juhudi kuunganisha umma dhidi ya chuki ya pamoja na migogoro ameendelea.

 utu wa kibinadamu unaweza kupatikana tu kwa kuheshimu jirani 

Bwana de Varennes amesema utu wa kibinadamu unaweza kupatikana tu kwa kuheshimu jirani , pamoja  na walio wachache na kwamba ili kila mtu  aweze kupata utu wa kibinadamu, serikali zinawajibika kuheshimu  haki za binadamu.

Mwezi juni mwaka 2016, shirika la Umoja wa Mataifa  linalohudumia  wakimbizi, UNHCR,  lilizindua kampeni kupitia mtandao wa Twitter, #WithRefugees ikimaanisha Pamoja na wakimbizi ikizitaka serikali kuazimia kutoa elimu kwa watoto wa wakimbizi, maji safi kwa familia za wakimbizi, na pia kuwapatia wakimbizi uhuru wa kuchangia katika jamii ili kuboresha stadi  zao mpya.