Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mauaji, utesaji, watu kutoweka na ukiukaji mwingine wa haki, bado ni tishio Burundi:UN

Waandamanaji wakiinuwa mikono juu ishara ya kujisalimisha kwa polisi katika kaya ya Musaga Bujumbura, Burundi
IRIN/Phil Moore
Waandamanaji wakiinuwa mikono juu ishara ya kujisalimisha kwa polisi katika kaya ya Musaga Bujumbura, Burundi

Mauaji, utesaji, watu kutoweka na ukiukaji mwingine wa haki, bado ni tishio Burundi:UN

Haki za binadamu

Tume maalumu iliyoundwa na baraza la haki za binadamu la  Umoja wa Mataifa kuchunguza visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Burundi imesema mauaji, uteseji, watu kutoweka na ukiukwaji mwingine bado vinaendelea na kuwa ni tishio kubwa kwa hatma ya haki nchini humo.

Katika ripoti yake iliyowasilishwa leo kwenye baraza la haki za binadamu mjini Geneva Uswis, tume hiyo imebainisha kuwa asilimia kubwa ya ukiukwaji huo unavihusisha vyombo vya usalama na wanamgambo wa Imbonerakure.

Matokeo ya ripoti hiyo yametokana na miezi mitatu ya kukusanya taarifa na ushahidi katika nchi za Ethiopia, Ubelgiji, Uganda,Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC na Rwanda , ambapo wataalam , waathirika na mashahidi wa ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Burundi wameelezea kuendelea kuwepo kwa ukiukwaji wa haki za binadamu na kuifanya mahakama ya kimataifa ya kimataifa ya uhalifu kuonyesha nia ya kuimarisha ushirikiano wake na tume tume hiyo.

Kutokana na ushahidi uliopatikana tume inaendelea na msimamo wake kuhusu ukiukwajii wa haki za binadamu  Burundi hasa kwa matukio ya  unyongaji wa watuhumiwa bila hukumu ya mahama, kutoweka kwa wanaharakati wa haki za binadamu, mateso na manyanyaso kwa wapinzani, kwa watu  wanaopinga uamuzi wa bunge kuhusu katiba mpya inayompa rais na chama chake mamlaka zaidi, ukiukwaji wa uhuru wa kiraia na haki za kiuchumi na kijamii.

Bw. Doudou Diene, ambaye ni mwekiti wa tume hiyo inayochunguza ukiukwaji wa haki nchini  Burundi  amesema  kuendelea kukiuka haki za bindamu, pamoja na kutotoa ushirikiano wa kuwafikisha wahusika katika mahakama ya kimataifa , Burundi inaenda kinyume na  azimio namba 36/19 la septemba mwaka 2017.

Sauti ya Doudou Diene

Ukiukwaji huo unawajumuisha pia kuwekwa rumande kwa wananchi wa Burundi  ambao walipinga mchakato wa katiba mpya. Na tuna ushahidi wa kutosha kuhusu matukio ya kukamatwa kwao. Na vitendo hiyv ovya  ukamataji vilifanywa kwa kutumia ubabe na chakusikitisha zaidi ni kwamba kuna matukio ya wananchi kutoweka.

Ameongeza kuwa wengi wanaotoweka sasa hata miili yao haipatikani

Sauti ya Doudou Diene-2

Hapo awali watu walipokuwa wanatoweka ,mara kadha tulikuwa na ushahidi kwasabau miili yao ilikuwa inapatikana, lakinikwa sasa kuna mbinu mpya ambapo miili yao inapotea kabisa  kusikojulikana

Ripoti imebaini kuwa ukiukwaji huu unawezeshwa na mazingira ya vitisho kutoka kwa viongozi ambapo  mwezi  Novemba mwaka 2017, Rais wa Jamhuri ya Burundi , katika hotuba kwa Siku ya mashuja, aliahidi “kusahihisha" wale wote ambao hawazingatiimisingi ya  chama.

Na mnamo tarehe 12 Desemba 2017, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya rasimu ya Katiba mpya, Rais huyo alitoa onyo kwamba"wote watakaojaribu kupinga  mchakato  huo watashughulikiwa”

Vivyo hivyo, mnamo tarehe 2 Mei 2018, alitangaza katika hotuba iliyofanyika Gitega akisema " Ikiwa wewe ni mzawa au mgeni, mtu yeyote anayepinga uchaguzi huu, nawaambieni, atapaswa kushindana na Mungu, aliye mbinguni, ni shahidi kwa hili. Lakini najua kuwa watu wengine ni viziwi wa kusikia ujumbe huu, waacheni  wanijaribu tu”

Tume pia imepata taarifa kuhusu watu ambao walitoweka kwa sababu ya kukataa kujiunga na chama tawala cha CNDD-FDD  naserikali ya Burundi bado imegoma  kutoa ushirikianno wakutosha kwa tume hiyo ili kufanikisha uchunguzi wake ili kuwezakuwafikisha wahusika katika vyombo vya dola.