Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MKUTANO WA 73 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA

MKUTANO WA 73 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA
MJADALA MKUU WA UNGA73

Mkutano wa 73 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaanza mwezi huu wa Septemba hadi wiki ya pili ya mwezi Septemba mwakani. Katika ukurasa huu hata hivyo tutakuwa tunakuletea habari motomoto kutoka mjadala wa wazi na vikao vya ngazi ya juu vya mkutano huo ambavyo vinafanyika kuanzia tarehe 25 septemba 2018 hadi Oktoba mosi 2018. Pamoja na hotuba za viongozi ni vikao vya ngazi ya juu kuhusu Kifua Kikuu, Ulinzi wa Amani, tukio maalum la kumuenzi hayati Nelson Mandela na magonjwa yasiyo ya kuambukiza, NCDs.

Taasisi ya Nelson Mandela/Matthew Willman

Madiba hakupenda makuu

Ikiwa leo Umoja wa Mataifa  unafanya tukio maalum kuhusu miaka 100 tangu kuzaliwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, hayati Nelson Mandela, mwanadiplomasia nguli nchini Tanzania na ambaye amewahi kuhudumu barani Afrika na Umoja wa Mataifa amemmwagia sifa hayati Mandela akisema kuwa alikuwa kiongozi shupavu ambaye kisasi chake baada ya kufungwa kilikuwa ni kuona watu wake wanaendelea.

Sauti
2'42"
UN

Viongozi wa sasa waige mfano wa Mandela- Dkt. Salim

Mwendazake Mzee Nelson Mandela, angalikuwa anatimiza umri wa miaka 100 mwaka huu iwapo angalikuwa hai. Ingawa hayupo, bado kile alichokifanya wakati wa uhai wake kinakumbukwa na kuenziwa siyo tu nchini mwake na barani Afrika bali pia katika Umoja wa Mataifa ambako ajenda alizokuwa anatetea ni mambo ambayo ni msingi wa Umoja wa Mataifa.

Sauti
4'31"