Pamoja na debe linalopigwa mafanikio kupambana na tabia nchi ni hafifu:Espinosa

9 Septemba 2018

 Licha ya wito unaotolewa kila siku kuchukua hatua za kutekeleza mkakati  madhubuti wa mabadiliko ya tabia nchi bado mafanikio ni hafibu.

Hayo yameelezwa katika taarifa iliyotolewa leo Jumapili mjini Bankok Thailand na ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na  mkutano wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchiUNFCCC, kwenye mkutano wa baraza Asia kuhusu mabadiliko ya tabia nchi.

UNFCC imesema muongozo wa utekelezaji unahitajika na muongozo huo umekuwa ukijadiliwa tangu 2016, na unatarajiwa kupitishwa katika mkutano wa kila mwaka wa mabadiliko ya tabia nchi , COP24 utakaofanyika Katowice, Polan mwezi Desemba mwak huu.

Akizungumzia kilichojiri kwenye mkutano huo wa Bankok, Bi Patricia Espenosa mkuu wa UNFCCC amesema hatua zilizopigwa zinatofautiana katika vita dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi na kwamba nchi zinaendelea na vita hivi.

Ameongeza kuwa hii inadhihirisha haja ya kuongeza juhudi za vita hivyo katika wiki zijazo. Mkutaba wa Paris wa mabadilikoya tabia nchi unahimiza kwamba nchi zichukue hatua ikiwemo kuongeza juhudi za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi kuongeza msaada kwa nchi zinazoendelea hasa ufadhili , teknolojia na kuwajengea mnepo wa kukabili mabadiliko ya tabia nchi.

Bi Espinosa amesema mkataba wa Paris, ni chombo cha mizania cha kuyaleta pamoja  mataifa yote. “ Ni lazima tutambue kuwa nchi zina hali tofauti nyumbani,” amesema . Na kuongeza,”Nchi zina viwango tofauti vya maendeleo ya kiuchumi na kijamii ambavyo husababisha hali tofauti za kitaifa jambo ambalo linafaa kutiliwa maanani wakati wa kutekeleza miongozo inayopangwa.”

Pia ametoa wito kwa viongozi wa kisiasa kusaidia kutatua masuala haya mapema kabla ya mkutano wa COP24.

Akiongeza kuwa mwaka huu ulimwengu umeshuhudia vifo kutokana  na mafuriko, ukameumekatili maisha ya watu wengi pamoja na miundombinu kadhaa kusambaratika katika mataifa yanayoinukia pamoja na yaliyoendelea.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter