Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MKUTANO WA 73 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA

MKUTANO WA 73 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA
MJADALA MKUU WA UNGA73

Mkutano wa 73 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaanza mwezi huu wa Septemba hadi wiki ya pili ya mwezi Septemba mwakani. Katika ukurasa huu hata hivyo tutakuwa tunakuletea habari motomoto kutoka mjadala wa wazi na vikao vya ngazi ya juu vya mkutano huo ambavyo vinafanyika kuanzia tarehe 25 septemba 2018 hadi Oktoba mosi 2018. Pamoja na hotuba za viongozi ni vikao vya ngazi ya juu kuhusu Kifua Kikuu, Ulinzi wa Amani, tukio maalum la kumuenzi hayati Nelson Mandela na magonjwa yasiyo ya kuambukiza, NCDs.

Ugonjwa wa TB si kulogwa, muhimu ufuate masharti ya matibabu -DJ Choka.

Ripoti ya Shirika la Afya Duniani WHO iliyotolewa hivi karibuni inaonyesha kuwa ugonjwa wa Kifua Kikuu  ndio unaongoza kwa kuwa ugonjwa hatari zaidi wa kuambukiza duniani. Takwimu za hivi karibuni zaidi za Umoja wa Mataifa zinasema kuwa hivi sasa watu milioni 10.4 duniani kote wameambukizwa ugonjwa huo huku milioni 1.6 wakifariki dunia kila mwaka. Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la afya .WHO linataka mbinu mtambuka za kuondokana na ugonjwa huu ifikapo mwaka 2030. Miongoni mwa mbinu hizo ni kutumia manusura wa ugonjwa huo kama wajumbe wa kuelimisha jamii ili ijikinge au isake tiba.

Sauti
3'27"