Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ahadi ni deni Niger yaikumbusha UN

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Niger, Kalla Ankourao, akihutubia mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kikao cha 73
UN Photo/Cia Pak
Waziri wa mashauri ya kigeni wa Niger, Kalla Ankourao, akihutubia mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kikao cha 73

Ahadi ni deni Niger yaikumbusha UN

Masuala ya UM

Serikali ya Niger imeukumbusha Umoja wa Mataifa kutekeleza mabadilliko katika mfumo wa vikosi vya Umoja huo vya kulinda amani kutoka nchi tano za Sahel vijulikamavyo kama G5.

Akizungumza katika mjadala wa wazi wa Baraza Kuu kikao cha73, Waziri wa mambo ya nje, ushirikiano na utangamano wa kikanda wa nchi hiyo, Kalla Ankourao, leo Jumamosi amesema kunoreshwa kwa vikosi hivyo kutasaidia kuimarisha ulinzi na usalama lakini pia kukabili changamoto ya ugaidi inayochochewa na kundi la Boko Haram.

Pia amesema kutaimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo tano za G5 Sahel ambazo ni Mali, Burkina Fasso, Chad, Mauritania na Niger katika kupambana na changamoto zingine mbali ya usalama kama mabadiliko ya tabia nchi, uhamiaji na njaa kwenye ukanda wa Sahel.

 Waziri wa Niger, amefafanua kuhusu kauli hiyo akimaanisha kuwa ni katika kuimarishwa kwa ushirikiano baina ya Umoja wa Mataifa na mashirika ya kikanda pamoja na mataifa yanayochangia askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa ndiyo ndio njia moja wpo ambayo itasaidia kuhakikisha kuwa vikosi hivyo  vinatumwa na pia kupewa uwezo kamili kwa kila aina ya mgogoro.

Waziri huyo pia, ametoa wito wa haraka kwa wadau walioahidi kutoa mchango wa fedha katika mkutano uliofanyika mwaka huu nchini Ubelgiji, kwa ajili ya kikosi kipaya cha pamoja cha Sahel ili kuhakikisha ufanisi katika utendaji wake.

Akigeukia suala la uhamiaji ambalo limekuwa mtambuka kwa vijana wengi kutoka Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kutumia Niger kama moja ya vituo vya kwenda kusaka maisha Ughaibuni na wengi kupoteza maisha jangwani na bahari ya Mediterranea amesema ni suala linalohitaji mshikamano wa kimataifa na Niger inaunga mkono mkataba wa kimataifa wa ujamiaji utakaokamiliswa Desemba huko Morocco ambako Niger itashiriki.

Waziri wa Niger amepongeza hatua zilichukuliwa katika eneo la pembe ya Afrika baina ya Ethiopia na Eritrea na pia mkataba wa kusitisha uhasama baina ya mahasimu wakuu nchini Sudan Kusini.

Nako Mashariki ya Kati amesema kuwa Niger inashikamana na watu wa Palestina kwa kutoka kufurahia haki zao za kuwa na taifa lao huru kufuata mipaka ya Juni 1967 na Jerusalem Mashariki kuwa ndiyo mji mkuu wa taifa lao.