Vita vyetu dhidi ya ugaidi vinakaribia ukingoni: Syria

29 Septemba 2018

Naibu waziri mkuu na waziri wa mambo ya nje wa Syria Walid al-Muallem amesema vita vya nchi yake dhidi ya ugaidi vinaelekea ukingoni akishukuru ujasiri, dhamira, umoja wa watu wa Syria, jeshi la nchi hiyo, msaada wa marafiki na washirika wao.

Katika hotuba yake kwenye mjadala wa wazi wa Baraza Kuu kikao cha 73 , Al-Moallem amesema imejizatiti kuendelea na vita hivyo

“Licha ya mafanikio haya , tumedhamiria kuendelea na vita hivi vitakatifu hadi pale maeneo yote ya Syria yatakapokombolewa kutoka mikononi mwa ugaidi wa aina zote na vikosi vyote haramu vya kigeni , kuwa huru dhidi ya mashambulizi yoyote toka nje, shinikizo au uzushi na madai. Ni wajibu wetu na haki yetu isiyo na mjadala , kama vile tulivyo ukomesha ugaidi katika maeneo mengi ya Syria.”

Ameongeza kuwa hali  hivi sasa nchi Syria imetengamaa kwa ajili ya wakimbizi wa Syria kurejea kwa hiyari “kwenye makazi yao waliyoyakimbia kwa sababu ya ugaidi na hatua za kiuchumi zilizowalenga katika mambo ya msingi ya uhai na maisha yao na kwamba maelfu ya raia wa Syria wamesharejea nyumbani.

Idlib nchini Syria kama ilivyo September 2018
WFP/Photolibrary
Idlib nchini Syria kama ilivyo September 2018

Ameongeza kuwa “kurejea nyumbani kwa kila raia wa Syria ni kipaumbele cha serikali ya nchi yetu na kwamba milango iko wazi kwa raia wote walioko nje kurejea nyumbani kwa hiyari na usalama.”

Licha ya mafanikio yaliyopatikana waziri huyo amesisitiza umuhimu wa kusongesha mbele mchakato wa kisiasa huku wakilinda haki, uhuru na hadhi ya taifa la Syria.

Al-Moallem ameweka bayana kwamba uwepo wa watu kutoka nje katika ardhi ya Syria bila ridhaa ya serikali “ni haramu na ni ukiukwaji wa sherika za kimataifa , katiba ya Umoja wa Mataifa na ni mashambulizi dhidi ya uhuru wa kitaifa pamoja, lengo la kupambana na ugaidi na tishio la amani na usalama katika kanda hii”.

Amesisitiza kwamba serikali yake inachukuliwa uwepo wa vikosi vyovyote katika himaya ya Syria bila ombi lao, ikiwa ni pamoja na majeshi ya Marekani, Ufaransa, na Uturuki vinachukuliwa katika muktada huo na hivyo ni lazima vikosi hivyo viondoke mara moja bila masharti yoyote.

 

 

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter