Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhamiaji Afrika si karaha bali ni faida:UNCTAD

Dkt. Mukhisa Kituyi, Katibu Mkuu wa UNCTAD. (Picha:UNCTAD/Nicholas Simiyu)

Uhamiaji Afrika si karaha bali ni faida:UNCTAD

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Kuuchukulia uhamiaji kama ni tatizo si fikra nzuri , kwani unahamiaji una faida nyingi, kwa wahamiaji wenyewe lakini pia kwa jamii zinazowahifadhi, iwe katika masuala ya kiuchumi, utamaduni na hata maendeleo kwa mujibu wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo UNCTAD

Suala la uhamiaji barani Afrika linapaswa kuchukuliwa kama ni fursa ya kupanua wigo wa maendeleo na sio mgogoro unaosababisha hasara na mtafaruku katika jamii. Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo UNCTAD.

Dkt. Mukhisa Kituyi ameyasema hayo alipozungumza na Flora Nducha kabla ya mjadala wa ngazi ya juu kuhusu mabadiliko ya mundo na uhamiaji barani Afrika utakaofanyika kesho Jumanne, anaanza kwa kueleza lengo la mabadiliko hayo ya kimuundo wanayotaka kuona..

(MAHOJIANO NA DKT. MUKHISA KITUYI)