Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushirikiano wa kimataifa ndio suluhu ya changamoto zinazotukabili:Espinosa

María Fernanda Espinosa Garcés;Rais wa kikao cha 73 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa , akizungumza wakati wa ufunguzi wa mjadala wa wazi wa Baraza hilo
Picha na UN/Cia Pak
María Fernanda Espinosa Garcés;Rais wa kikao cha 73 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa , akizungumza wakati wa ufunguzi wa mjadala wa wazi wa Baraza hilo

Ushirikiano wa kimataifa ndio suluhu ya changamoto zinazotukabili:Espinosa

Masuala ya UM

Misingi mikuu mitatu ambayo ni uongozi bora, kushirikiana majukumu na kuchukua hatua za pamoja ni muhimu kwa mustakhbali wa dunia amesema Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Maria Espinosa.

Ili tuweze kukabili ipasavyo changamoto zinazotukabili, tunahitaji ushirikiano wa kimataifa.

Wito huo umetolewa leo na Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa María Fernanda Espinosa wakati wa ufunguzi wa mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kikao cha 73 mjini New York Marekani.

Rais huyo amewasihi viongozi wa dunia kudumisha umoja, na kufanya kazi pamoja katika juhudi za kuelekea utimizaji wa malengo ya maendeleo endelevu SDG’s na kuhakikisha usawa kwa wote.

 

Bi. Espenosa amesisitiza kuwa mchango wa Umoja wa Mataifa katika utu wa binadamu umekuwa mkubwa , akikumbushia misingi inayoongoza chombo hicho cha kimataifa  na kusema” Ukweli ni kwamba kazi ya Umoja wa Mataifa inasalia kuwa muhimu leo hii kama ilivyokuwa miaka 73 iliyopita . Ushirikiano wa kimataifa ndio jibu pekee linalowezekana kwa changamoto zinazotukabili. Kuudhoofisha au kuhoji kuhusu mshakamano huo hakutoleta tija yoyote badala yake kutazusha tafran, kutoaminiana na mkwamo katika masuala ya muhimu.”

Akigeukia masuala ya kipaumble katika Baraza Kuu miaka ijayo amesema usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake, utekelezaji wa mkataba wa kimataifa wa wahamiaji na wakimbizi, kuhakikisha fursa za kazi zenye hadhi kwa wote , utekelezaji wa mkataba wa mabadiliko ya tabia nchi na mazingira.