Viongozi wa sasa waige mfano wa Mandela- Dkt. Salim

Viongozi wa sasa waige mfano wa Mandela- Dkt. Salim

Pakua

Mwendazake Mzee Nelson Mandela, angalikuwa anatimiza umri wa miaka 100 mwaka huu iwapo angalikuwa hai. Ingawa hayupo, bado kile alichokifanya wakati wa uhai wake kinakumbukwa na kuenziwa siyo tu nchini mwake na barani Afrika bali pia katika Umoja wa Mataifa ambako ajenda alizokuwa anatetea ni mambo ambayo ni msingi wa Umoja wa Mataifa.

Misingi hiyo ni utetezi wa haki za binadamu na kusaka amani bila vurugu. Kwa kuzingatia hilo, Umoja wa Mataifa umefanya tukio maalum la kumuenzi kwa kupitisha azimio la kisiasa la kutambua mchango wake katika kutetea haki za binadamu na amani kote ulimwenguni. Lakini hayati Mandela alikuwa ni mtu wa namna gani? Stella Vuzo wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa huko Dar es salaam Tanzania amezungumza na Dkt. Salim Ahmed Salim, mwanadiplomasia nguli ambaye aliwahi kufanya naye kazi wakati Dkt, Salim akiwa Katibu Mkuu wa uliokuwa Umoja wa nchi huru za Afrika OAU sasa Muungano wa Afrika, AU. Dkt. Salim anaanza kwa kuzungumzia anamkumbuka vipi.

Soundcloud
Audio Credit
Siraj Kalyango/Stella Vuzo
Audio Duration
4'31"
Photo Credit
UN